Halima Mdee na wenzake 18 hawana nguvu yoyote ya kimaamuzi Bungeni, wanaburuzika tu

Nauchukia sana mfumo wetu. Unawafanya wananchi wasiihoji serikali yao, hasa kwenye majukwaa yalio rasmi kama bungeni .

Huu mfumo waTz watakuja kugundua wakiwa wamechelewa sana.

Nb mtuma thread ni johnthebaptist . Haeleweki
Huku vijijini wananchi wanahoji sana bwashee.

Tatizo ni huko juu yaani bungeni nk wanakosubiria teuzi!
 
Magufuli alitenda kama tuko katika mfumo wa chama kimoja, na huo ndio ukweli vyama vingine vyote ni matawi ya CCM!
Kwa hiyo katika hili, kama mada yako inavyoainisha, Magufuli asingeweza kusema lolote maana bunge hili lililojaa wana CCM ni zao lake.
 
Huku vijijini wananchi wanahoji sana bwashee.

Tatizo ni huko juu yaani bungeni nk wanakosubiria teuzi!
Vijijini wana maamuzi gani?!. Niliwahi kuwepo Geita, wakati mzee wa ukweli na uwazi ana binafsisha migodi. Maamuzi yalitoka juu vijiji vilishirikishwa ktk hatua za mwisho tena si kwa maamuzi, bali taarifa na ushauri wafanye nini
 
Unataka wafanye maamuzi wafurushwe bungeni? Wabunge wa COVID-19 ni tatizo kwa bunge
 
Huku vijijini wananchi wanahoji sana bwashee.

Tatizo ni huko juu yaani bungeni nk wanakosubiria teuzi!

Vijijini wanamuhoji nani mzee?

Kikatiba bunge ndio baraza kuu na rasmi lenye mamlaka ya kuweza kuihoji serikali, na kuisimamia...

Hao wa vijijini sauti zao zinaishia huko huko...
 
Vijijini wana maamuzi gani ?!. Niliwahi kuwepo Geita , wakati mzee wa ukweli na uwazi ana binafsisha migodi. Maamuzi yalitoka juu vijiji vilishirikishwa ktk hatua za mwisho tena si kwa maamuzi, bali taarifa na ushauri wafanye nini
Unazungumzia miaka 20 iliyopita?

Karibu leo!
 
Hivi Mzee Mgaya ndiye Yohana Mbatizaji au tumngojee mwingine?
 
Vijijini wanamuhoji nani mzee?

Kikatiba bunge ndio baraza kuu na rasmi lenye mamlaka ya kuweza kuihoji serikali, na kuisimamia...

Hao wa vijijini sauti zao zinaishia huko huko...
Vijijini wanazihoji serikali zao.

Serikali inasimamiwa na CCM siyo bunge.

Spika ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM ambayo Rais ndio mwenyekiti wake.
 
Vijijini wanazihoji serikali zao.

Serikali inasimamiwa na CCM siyo bunge.

Spika ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM ambayo Rais ndio mwenyekiti wake.

Serikali inasimamiwa na CCM??? kwa heri...
 
Kuna watu mkishalewa huwa mnajisahaulisha! Ina maana manunuzi ya wapinzani na uchafuzi wa 2020, hukuwepo Tanzani?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…