Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
HALIMA MDEE NA MWENZAKE 18 WAMEJIMALIZA KISIASA.
Habari za siku za mwisho wa wiki Wajumbe wa JF,
Hakikaki katika kitu ambacho hua naamini kwenye maisha yangu ni kwamba njia ya mkato kwenye maisha huleta mafanikio ya muda na hatimaye baadae kuacha katika matatizo makubwa sana.
Ndugu Halima Mdee na kundi lake la Wanawake 18 ambao wengi wao bado ni wanasiasa vijana miaka 30-45, bila kupima maumivu ya baadae kwenye kesho yao wamejitia kiburi kujimaliza kisiasa pasipo kujali maelekezo ya waliokua viongozi wao. Wanaenda kujimaliza kisiasa mapema ikiwa bado siasa zinawahitaji sana leo na kesho.
NI VIPI KINAMAMA HAWA WANAJIMALIZA KISIASA?
Ikumbukwe kwamba kinamama hawa bado wanahitaji maisha marefu ya kisiasa. Hawataweza kupata umaarufu katika chama chochote kwa sasa na hata baada ya 2025 jambo walikua nao wakiwa CHADEMA.
Waliota ndevu kwa kudhani kwamba wana jasho lako kubwa katika chama hicho wakidhani walikosea hawawezi kuguswa wakasau kua chama hicho kimekuwa taasisi kubwa yenye wanachama na wafuasi wengi nchi nzima.
Mdee na kundi lake wanachoweza kuambulia kwa sasa ni ubunge wao wa kulindana walioahidiwa na Ndungai ambaye hajali katiba ya nchi kwajitamba na vikanuni vyake vya bunge. Baada ya 2025 hawa kinamama hata walihamia CCM kwenda kufanya siasa mpya kwa kugombea kwenye majimbo haitowezekana kwa vile majimbo yote yote bado yapo chini ya CCM, hivyo kumtoa mbunge wa ccm aliyepo kwenye jimbo si rahisi.
Kwenda kugombea viti maalum ndani ya CCM si rahisi kwa maana zile nafasi zinahitaji uzoefu wa ndani ya chama muda mrefu wajumbe wakuzoee.
Wanachoweza kupata zaidi kwa mapenzi ya Rais ajaye ndani ya CCM labda kuu wa Wilaya, Mkoa, Ukatibu tawala au Ukurugenzi na Ubalozi ambapo bado itategemea na mapenzi ya Rais ajaye kupitia CCM kwenye demokrasia ya nchi Maana si wanaccm wote wanafurahia hawa na anayofanya Magufuli.
LABDA WANAWEZA KUHAMIA VYAMA VIINGINE VVYA UPINZANI?
Si rahisi sana kwa kinamama hawa kwenda kupata umaarufu kwenye vyama vipya vya upinzani kama ilivyokua kwa CHADEMA ambacho kiko kwenye Consistency ya Upinzani imara kwa miaka 20 sasa. Hivi vyama viingine vya upinzani bado vinahitaji kujengwa haviwezi kumpa mtu umaarufu wa haraka hivyo.Kwahiyo si rahisi sana kwenda kuwika kwenye vyama vingine vya siasa mapema hivyo, inahitaji kwanza muda kujijenga upya.
Kwa sasa watapambwa na kuchonganishwa sana na wanaccm maana wanatamani CHADEMA ife leo, wanaccm hawawaonei huruma kinamama hawa, nia yao ni kutaka kuona upinzani wa kughushi bungeni ili mambo yao yaendelee hasa kwenye mashinikizo yaliyopo hivi sasa ya jumuiya za kimataifa.
NINI CHA PEKEE WAFANYE ILI WAJINUSURU NA HALI HII?
Mimi kama mwanasiasa mkongwe, mwandishi na mchambuzi wa siasa ndani ya nchi yangu, njia pekee ya kinamama hawa kurudi kwenye siasa ni kuandika barua kwa viongozi wao wa zamani wa CHADEMA wakiwaomba radhi na wajiondoe kwenye nafasi hizi za ubunge wa muda ambao lengo lake ni kuinufaisha serikali ya CCM na Chama chenyewe. Faida ya kufanya hivi ni kubwa kuliko kwenda kuanza maisha mapya kwenye vyama vipya.
Asiogope kua wanachama watakosa imani nao, wao ni wakongwe kwanza ndio wataibua furaha kubwa kwa wanachadema kwa ujasiri wa kuomba radhi maana hakuna asiyekosea.Kwa kufanya hivi maisha yanasonga mbele na nyota zao za kisiasa zitazidi kung'ara zaidi. Kama wewe ni mwanachama ni mwanachama tu haijalishi ukikosea kiasi gani.
Kama hawaamini katika hili wawaulize Mama Sophia Simba wa CCM aliyefukuzwa uanachama CCM na kisha baadaye kuomba radhi na leo hii ni mbunge tena. Watazame kina Nape Nnauye na Makamba maisha yanaendelea na siasa zao zinaendelea haijalishi walikosea kiasi gani.