Halima Mdee na wenzako endelea na ubunge mmeshaahidiwa kulindwa

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Ndugu wana COVID-19, nawasilimu

Kwa sisi tuliowatangulia huku kitaa, Tunajuwa maisha yalivyo magumu kwa Sasa, na tunafahamu Ni kwa kiasi gani mmepata ugumu pale mlipohakikishiwa kuwa mnarudi bungeni kwenye maisha ya mshahara na posho, maisha ambayo wengi wenu mlikuwa mmeyazoea na yalikuwa yameyeyuka tarehe 28 October 2020.

Kwa kigezo Cha maisha yalivyo magumu huku mitaani, Mimi siwezi kuwalaumu kwa sababu natambua kuwa mmewaza juu ya mshahara na posho anazopata Mbunge Kisha mziache na kuja kupigana na mtaa kwa miaka mitano chini ya anayejiita Jiwe, Hali ingekuwa ngumu zaidi.

Kwa kuwa mmeshaambiwa mtalindwa na hivyo Basi mna uhakika wa miaka mitano, Basi hakuna haja ya kuhangaika kuita vyombo vya habari ili kujitetea au kutupiga swaga vijana wanasema.

Kila mwenye akili timamu anajuwa kikubwa mmethamini posho kuliko utu na heshima mliyojijengea kwa kipindi kirefu, lakini haya yote yanaweza yasiwe na maana Kama tu utaangalia upande wa pesa.
Hongereni kwa kurudi bungeni.

Sisemi pigeni kazi Bali nitasema pigeni pesa maana nyie hamjasukumwa na kupiga kazi Bali kupiga pesa.

Kila la heri kwenye upigaji
 
Hao wasizuiwe kwenye hiyo press conference maana wanaweza kujifanya wana la maana, waachwe waitishe hiyo press wamwage hasira zao zote. Aliitisha press Dr. Slaa na hakuna mtu alimfuata, na bado hadi leo ccm bado wanategemea wizi wa kura na umwagaji damu ili kukaa madarakani, ndio itakuwa hao wahuni wachache.
 
Da hii ni speed halali ya dunian watu wanaitwa COVD -19 sasa
 
Ndugu wana COVID-19, nawasilimu

Kwa sisi tuliowatangulia huku kitaa, Tunajuwa maisha yalivyo magumu kwa Sasa, na tunafahamu Ni kwa kiasi gani mmepata ugumu pale mlipohakikishiwa kuwa mnarudi bungeni kwenye maisha ya mshahara na posho, maisha ambayo wengi wenu mlikuwa mmeyazoea na yalikuwa yameyeyuka tarehe 28 October 2020.

Kwa kigezo Cha maisha yalivyo magumu huku mitaani, Mimi siwezi kuwalaumu kwa sababu natambua kuwa mmewaza juu ya mshahara na posho anazopata Mbunge Kisha mziache na kuja kupigana na mtaa kwa miaka mitano chini ya anayejiita Jiwe, Hali ingekuwa ngumu zaidi.

Kwa kuwa mmeshaambiwa mtalindwa na hivyo Basi mna uhakika wa miaka mitano, Basi hakuna haja ya kuhangaika kuita vyombo vya habari ili kujitetea au kutupiga swaga vijana wanasema.
Kila mwenye akili timamu anajuwa kikubwa mmethamini posho kuliko utu na heshima mliyojijengea kwa kipindi kirefu, lakini haya yote yanaweza yasiwe na maana Kama tu utaangalia upande wa pesa.
Hongereni kwa kurudi bungeni.

Sisemi pigeni kazi Bali nitasema pigeni pesa maana nyie hamjasukumwa na kupiga kazi Bali kupiga pesa.
Kila la heri kwenye upigaji

Hakuna utu bila pesa. Acha wapige pesa kuinua utu wao ili waweze kuwakilisha wananchi bila stress na depression.

Halima oyee!
 
Ni kweli cha muhimu ni kukaa kimya kula hiyo hela chini ya ulinzi wa Ndugai mvunja katiba ya nchi!
 
Back
Top Bottom