Halima Mdee: Sisi ni wawakilishi wa chama na hatukuja Bungeni kwa bahati. Nafasi zetu za Ubunge hazipo hatarini hata kiduchu

Anawakilisha chama gani? Ambacho kimemfukuza uanachama au Kuna kingine?
HII NCHI NGUMU SANA VIONGOZI WETU WANAWEZA KUISHI HATA JEHANAMU BIKA WOGA
 
Kinachonifanya nifuatilie siasa ni maumivu ya kodi ninayolipa.
Huu mchezo wa hawa wabunge unasababisha watu kudemka mitandaoni. Wanakuwa declared na Baraza kuu kuwa wamefukuzwa na kama sikosei na mkutano mkuu baada ya kuchakata rufaa zao. Ingawa mimi si mwana sheria ula nijuavyo (naweza kusahihishwa) utaratibu ni kama wamekata rufaa wanaendelea kuwa wabunge hadi hivyo vikao vikao vyao vya kikatiba vitakapo toa maamuzi ya kuthibitisha au kubatilisha maamuzi ya vikao vya chini. Sasa ni lini hivyo vikao vimekaa na kutolea maamuzi rufaa zao? Kama havijakaa kwanini havikai kutoa maamuzi halafu tuone kama hawa wabunge wataendelea kuwa bungeni baada ya maamuzi ndo tuhoji?. Kweli hatudemki mitandoni tu wakati wnye chama wakitucheck kwa pembeni?
 
Esther Bulaya
Esther Matiko
Halima Mdee
Wamepotea kwenye siasa za upinzani [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hakuna anayemtishia,yeye aende,si wakala wa chama,anaogopa nini?
Hakuna kitisho, aende akapokelewe Kwa shangwe na Bawacha na Bavicha, Kwa uwakilishi wake mahiri WA chama!
Komedi za nchi hii haziwezi kuisha maana Matumbo shurti yajazwe
 
Ajitokeze kwenye kesi ya Mbowe huyu wakala wa chama,aone wafuasi wa hicho chama watamfanya nini.
Aje kufanya nini? hata kama ni mimi nisinge kuja. Yani aache PESA aje kwenye makelele.
 
Ila CCM lakini dah, kuna wakati unapata hasira sana ukiwaza siasa zao unafika wakati unaamua ufanye yako tu.

Unaweza kujikuta unapata hasira unaamua kuvaa mabomu uwalipue wote .
Uangalie tu eti Tulia kapata asilimia 100, asilimia ambazo hata Mwenyezi Mungu hawezi kuzipata, maana mpinzani shetani yupo. Sasa Hawa CCM asilimia mia wanazipataje?
 
Hiyo kauli imefunga mjadala.

Watu wasilazimishe sana hao kina mama wakafunguka maana kuna watu wataaibika.

Mashabiki wa Chadema mkubaliane tu na hali tuendelee na maisha.
Sijamsikia mtu akibembeleza wakae kimya. Chama chao cha zamani ndicho kilichomwandikia Spika aliyepita kumtaka aweke wazi utaratibu uliofuatwa mpaka hawa kuapishwa. Kwenye hili watakao umbuka ni wale walio wakingia kifua bila kujali Katiba inasemaje.

Amandla...
 
Mambo ya aibu
 
Kwani chama Chao kishawahi kukanusha kuwa kupitia hao wabunge 19, chama hakipati ruzuku toka serikalini?
 


Darmpya Blog

@darmpya_
· 17h
"Siamini kama nafasi zetu hapa bungeni ziko hatarini kwa sababu ya mabadiliko ya Spika,hatukuja hapa bungeni kwa bahati mbaya,sisi ni wabunge,tumeapa,ni wawakilishi wa chama, hivyo tunaendelea na kazi zetu kama kawaida"@halimamdee #BUNGENILEO
 
Kwani ulitaka au ulitegemea asemeje? Mfumo ambao uliwapeleka pale bado uko vilevile pamoja na kumeguka wakuu wawili wa mihimili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…