Halima Selengia mpigania uhuru na shujaa wa TANU

Halima Selengia mpigania uhuru na shujaa wa TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Kwa miaka mingi sana nimekuwa nikitafuta picha ya Bi. Halima Selengia wa Moshi mmoja wa akina mama waliokuwa waasisi wa TANU na wapigania uhuru wa Tanganyika.

Leo asubuhi nimepokea picha yake baada ya mawasiliano mafupi jana usiku na kijana wake ambae baada ya kusoma makala ambayo nilimtaja Bi. Halima, huyu kijana akaniandikia kwa hisia kubwa akinifahamisha kuwa nimemtajia mmoja wa wazee wake ambae yeye akimjua toka akiwa mtoto mdogo hadi anakua na kuwa kijana.

Tumshukuru sana ndugu yetu huyu kwa hisani hii kubwa na hidaya hii aliyotupatia.

Miongoni mwa matawi yote ya TANU nchini Tanganyika, tawi pekee lililoungwa mkono na wanawake na wao kuwa ndiyo nguvu kuu ya chama, lilikuwa tawi la TANU la Moshi mjini.

Nguvu kuu ya TANU ilikuwa wanawake wengi wao wakifanya biashara ndogo ndogo.

Tawi hili la Moshi mjini ndilo tawi lililomtoa Lucy Lameck ambae mji wa Berlin, Ujerumani umeamua kumpa barabara kwa mchango wake.

Hili tawi la Moshi mjini ndilo lilikuwa tawi la Bi. Amina Kinabo.

Nafasi ya wanawake katika harakati mjini Moshi inaweza kuonekana katika katika safari ya pili ya Julius Nyerere Kilimanjaro.

Katika safari hiyo Nyerere alifikia nyumbani kwa Bibi Halima Selengia aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya tawi la TANU Moshi.

Safari ya kwanza Nyerere alifikia KNCU Hotel (Hoteli ya Kilimanjaro Native Cooperative Union).

Wakati huo TANU ilikuwa haijaota mizizi.

Lakini katika safari yake ya pili wanachama walidai kwamba lazima Nyerere atayarishiwe malazi yake na TANU.

Hii ndiyo ikawa sababu ya Baba wa Taifa kufikia nyumbani kwa Bi. Halima Selengia.
 
Back
Top Bottom