Halima Selengia shujaa wa TANU na mpigania uhuru wa Tanganyika

Halima Selengia shujaa wa TANU na mpigania uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Kwa miaka mingi sana nimekuwa nikitafuta picha ya Bi. Halima Selengia wa Moshi mmoja wa akina mama waliokuwa waasisi wa TANU na wapigania uhuru wa Tanganyika.

Leo asubuhi nimepokea picha yake baada ya mawasiliano mafupi jana usiku na kijana wake ambae baada ya kusoma makala ambayo nilimtaja Bi. Halima, huyu kijana akaniandikia kwa hisia kubwa akinifahamisha kuwa nimemtajia mmoja wa wazee wake ambae yeye akimjua toka akiwa mtoto mdogo hadi anakua na kuwa kijana.

Tumshukuru sana ndugu yetu huyu kwa hisani hii kubwa na hidaya hii aliyotupatia.

Miongoni mwa matawi yote ya TANU nchini Tanganyika, tawi pekee lililoungwa mkono na wanawake na wao kuwa ndiyo nguvu kuu ya chama, lilikuwa tawi la TANU la Moshi mjini.

Nguvu kuu ya TANU ilikuwa wanawake wengi wao wakifanya biashara ndogo ndogo.

Tawi hili la Moshi mjini ndilo tawi lililomtoa Lucy Lameck ambae mji wa Berlin, Ujerumani umeamua kumpa barabara kwa mchango wake.

Hili tawi la Moshi mjini ndilo lilikuwa tawi la Bi. Amina Kinabo.

Nafasi ya wanawake katika harakati mjini Moshi inaweza kuonekana katika katika safari ya pili ya Julius Nyerere Kilimanjaro.

Katika safari hiyo Nyerere alifikia nyumbani kwa Bibi Halima Selengia aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya tawi la TANU Moshi.

Safari ya kwanza Nyerere alifikia KNCU Hotel (Hoteli ya Kilimanjaro Native Cooperative Union).

Wakati huo TANU ilikuwa haijaota mizizi.

Lakini katika safari yake ya pili wanachama walidai kwamba lazima Nyerere atayarishiwe malazi yake na TANU.

Hii ndiyo ikawa sababu ya Baba wa Taifa kufikia nyumbani kwa Bi. Halima Selengia.

Screenshot_20201129-082549.jpg
 
Nice history next time come with full info itakua nzuri zaidi tujue mchango wake ulikua kwenye nn na nn ama ameacha alama gan
 
Nice history next time come with full info itakua nzuri zaidi tujue mchango wake ulikua kwenye nn na nn ama ameacha alama gan


Historia za wanaharakati na wapigania uhuru wengi wa nchi hii zimefukiwa, inatakiwa watu wa kuifukua kama ndg Mohamed Said anavyofanya, nionavyo hii ni juhudi ya mtu binafsi.
 
Sijaelewa mchango wake ni kumpokea mahali pa kufikia au kuna cha ziada alifanya
 
Sijaelewa mchango wake ni kumpokea mahali pa kufikia au kuna cha ziada alifanya
Kazi...
Kaa uwaze na jiulize imewezekana vipi Nyerere Rais wa TANU afikie kwa Bi. Halima Selengia?

Kaa kitako tuliza akili zako jiulize ni watu gani walikuwa karibu ya Nyerere wakati wa kupigania uhuru?

Jiulize tena watu hawa waliokuwa bega kwa bega na Baba wa Taifa wakati wa kupigania uhuru walikuwa na hadhi ipi na heshima gani wakati wa kupigania uhuru?

Ukiwa hujapata jibu waulize watu huko mitaani watakufahamisha ni akina nani walijitolea kupigania uhuru wa Tanganyika wakiwa na Baba wa Taifa.

Hapo ndipo utaelewa mchango wa Mama bint Maalim, Amin Kinabo na Lucy Lameck.
 
Back
Top Bottom