Halitete: Ukimya wa wanaJF kutoa Mialiko serious ya Madikodiko ya PASAKA! Nini kimewakuta?

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,203
Reaction score
37,906
Salamu sana wanandugu?

JF ni Jumuiya kubwa sana! JF imekusanya watu wa nasaba mbali mbali! JF imebeba watu wa hadhi na rika mbali mbali! JF imebeba marafiki wa kweli, wa dhati, JF ina mpaka wanandoa wa kweli! JF ina watu wenye mahaba yao, achana na walioweka dhahiri shahiri kama Demiss na Mkuu sana, mtu kweli, mtu mara mbili Mshana Jr yote kwa yote JF ni kiwakilishi kizuri cha Jamii halisi ya Kitanzania.

Napenda kuhoji hapa, nini kimewakuta wanajamii sisi? Kulikoni mpaka sasa hakuna mualiko siriazi wala hakuna alietoa ramani halisi ya kutukaribisha ndugu na jamaa huko kwenye madikodiko, maanjumati, mapilau pilau?

Haiwezekani kuwa eti Majiko ya Wana JF leo hayapikiki? Sio kweli! Haiwezekani wanaJF wote leo mmealikwa, kwamba eti na nyinyi hamuwezi kualika mlikoalikwa! Shabash.... huu ukimya kuna nini huko? Mnakula nini hicho kisichofaa kuliwa na wote?

Humu JF kuna members ambao wao tu ni brand kubwa sana, inatisha kuona siku km ya leo wapo kimya, humu kuna wadada wa heshima kubwa kama Sky Eclat Sakayo Demiss mke wa Mshana Jr geniveros mumu Jolie Jolie NAHUJA Shunie

JF pia ina majembe yake, brand kubwa tu Mshana Jr GENTAMYCINE johnthebaptist Tairi bovu Mwifwa Mwana kondoo Quinine korojani IKIRIRI Erythrocyte MTAZAMO MSELA WA MANZESE Ningewataja wote, ila nina kibarua cha kupokea wageni hapa Kijijini kwangu!

On behalf of myself, pamoja nakusikitishwa na ukimya wenu Pasaka hii, nawakaribisha sana mje tujumuike ama laah, muda ndio huu, kwa heshima na taadhima, tumeni wawakilishi wenu, karibuni kwangu, Tubuyu, kama utapata tabu kufika piga simu 26-999, nitapokea mimi!
 

Attachments

  • chako.jpg
    9.4 KB · Views: 34
  • chamchana.jpg
    11.9 KB · Views: 35
  • chamgeni.jpg
    8.9 KB · Views: 31
  • jicho.jpg
    9.4 KB · Views: 31
  • kaatayari.jpg
    9.2 KB · Views: 32
  • kichuguu.jpg
    9.3 KB · Views: 34
  • kitu.jpg
    9.6 KB · Views: 28
  • tule.jpg
    7.6 KB · Views: 38
  • Ugali.jpg
    9.2 KB · Views: 31
  • utamu.jpg
    8.7 KB · Views: 28
Sa mbona mwenyewe haupo serious asee, nikipanda Bajaji nashukia wapi
 
Sa mbona mwenyewe haupo serious asee, nikipanda Bajaji nashukia wapi
Nipo siriaz wangu.... madereva wa bajaj mi washkaji, nasafiri kisela... waambie kwa slimTano!
 
Au Vyuma vimekaza...maana hata Mimi nashangaa Mpaka sahv Jirani yangu ...Ajaniletea hotpot la pilau wakati Mimi siku za IDD Uwa aizidi SAA 7 kamili sijamletea dishi lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…