ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha ACT-Wazalendo kinaendele muda huu Hoteli ya Lamada jijini Dar-es-salaam Tanzania.
Leo Halmashari Kuu inapitia na kupeleka majina ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Zanzibar kwa Mkutano Mkuu utakaofanyika Agosti 05, 2020 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall.
Aidha leo Agosti 3, 2020 Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe amemteua Ndugu Bernard Membe kuwa Mshauri Mkuu wa Chama. Pia amemteua, Wakili Emanuel Mvula kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.
Tayari viongozi hao wamethibitishwa rasmi na Halmashauri Kuu ya Taifa.
Arodia Peter
Afisa Habari wa ACT–Wazalendo
0717414278