KERO Halmashauri ya Bunda mjitafakari, msifanye kazi kwa mazoea

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Majitha

Member
Joined
Jan 4, 2016
Posts
17
Reaction score
8
Imenishangaza sana, niko hapa Bunda (Mkoani Mara) nina biashara yangu, jana nilienda Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Bunda ili kufanyiwa hesabu nilipe mapato na ushuru wa hotel (hotel levy), nikaambiwa wako kikaoni, mbali na kusubiri for 5 hours.

Baadaye nikaambiwa 'Tunaomba tu urudi kesho', leo nimeenda tena nimekuta Ofisi hiyo ya Serikali imefungwa na hakuna mtumishi hata mmoja, nikaambiwa na mlinzi njoo tena kesho.

Kinachonishangaza ni kuwa kwanini asibakishwe hata mtumishi mmoja wa kuwahudumia wananchi? Ofisi ya Serikali inafungwaje wakati wa saa za kazi na Wananchi wanakuletea mapato ya ushuru.

Hili linafikirisha sana, ninaomba watumishi waliopewa dhamana wajipime na kujitafakari kama wanaweza kuaminiwa kuendelea kukaa kwenye Ofisi za Serikali bila kuwatumikia wananchi.

20241211_110025.jpg
 
Mkuu hakuna kitu kinaniudh kama hiyo kodi ya hotel levy Yan kulipa 10% ya Kila mteja huu ni unyonyaji
 
Uhaba wa watumishi na kutoa ajira hawataki, kuendelea kufanya kazi kwa mazoea, hiyo kodi ya hotel levy nayo imekaa kinyonyaji sana kwa mfanyabiashara.
 
Imenishangaza sana, niko hapa Bunda (Mkoani Mara) nina biashara yangu, jana nilienda Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Bunda ili kufanyiwa hesabu nilipe mapato na ushuru wa hotel (hotel levy), nikaambiwa wako kikaoni, mbali na kusubiri for 5 hours.

Baadaye nikaambiwa 'Tunaomba tu urudi kesho', leo nimeenda tena nimekuta Ofisi hiyo ya Serikali imefungwa na hakuna mtumishi hata mmoja, nikaambiwa na mlinzi njoo tena kesho.

Kinachonishangaza ni kuwa kwanini asibakishwe hata mtumishi mmoja wa kuwahudumia wananchi? Ofisi ya Serikali inafungwaje wakati wa saa za kazi na Wananchi wanakuletea mapato ya ushuru.

Hili linafikirisha sana, ninaomba watumishi waliopewa dhamana wajipime na kujitafakari kama wanaweza kuaminiwa kuendelea kukaa kwenye Ofisi za Serikali bila kuwatumikia wananchi.

Pole sana lakini Hotel levy umefata nini ofisini? Wakati mfumo wa tausi portal unakuruhusu ujihudumie hata ukiwa nyumbani kwako muhimu u attach hayo mauzo Yako ya kitabu ukisa ume ya scan kwenye mfumo wa portal.
 
Back
Top Bottom