Pre GE2025 Halmashauri ya Jiji la Mbeya imependekeza kuanza mchakato wa kuligawa jimbo la Mbeya mjini kupata jimbo jipya la Uyole

Pre GE2025 Halmashauri ya Jiji la Mbeya imependekeza kuanza mchakato wa kuligawa jimbo la Mbeya mjini kupata jimbo jipya la Uyole

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wakuu

Halmashauri ya Jiji la Mbeya imependekeza kuanza mchakato wa kuchunguza na kuligawa Jimbo la Mbeya Mjini kupata jimbo jipya la Uyole, katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2025.

Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Dk Tulia Ackson ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU).

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mchakato huo ukikamilika na kukidhi vigezo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) italitangaza jimbo jipya, jambo ambalo litakuwa jawabu la matakwa ya wakazi wa Mbeya Mjini.

Kwako Stuxnet
 
Mbeya badala ya kuwaza maendeleo wao kila kukicha wanapewa mambo sijui kuigawa Songwe na Mbeya wamekubali sasa hivi Ubunge na miaka nenda rudi bara bara ni zile zile hakuna kitu kinafanyika wao wanawaza sana siasa bila vitendo.
 
Mbeya wamewekeza kwenye makanisa.

Wale Malafayale wa Mbeya Profesa Mwandosya na Dr Mwakyembe wanatoka ukanda mwingine.
 
Mbeya wamewekeza kwenye makanisa.

Wale Malafayale wa Mbeya Profesa Mwandosya na Dr Mwakyembe wanatoka ukanda mwingine.
Prof Mwandosya ndie alielazimisha kujengwa uwanja wa ndege wa Songwe ima wahuni hawakupenda wakampeleka mtu agombee kwenye ujumbe wa NEC ili kumtoa Prof kwa bahati nzuri alishinda kwa kura chache sana Mbeya hawajui wanataka nini wao wapo busy na Siasa mbovu hata kwa madhara ya Mkoa wao wao wanaona sawa tu.
 
Back
Top Bottom