Halmashauri ya Jiji la Mbeya imependekeza kuanza mchakato wa kuchunguza na kuligawa Jimbo la Mbeya Mjini kupata jimbo jipya la Uyole, katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2025.
Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Dk Tulia Ackson ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU).
Mchakato huo ukikamilika na kukidhi vigezo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) italitangaza jimbo jipya, jambo ambalo litakuwa jawabu la matakwa ya wakazi wa Mbeya Mjini.
Mbeya badala ya kuwaza maendeleo wao kila kukicha wanapewa mambo sijui kuigawa Songwe na Mbeya wamekubali sasa hivi Ubunge na miaka nenda rudi bara bara ni zile zile hakuna kitu kinafanyika wao wanawaza sana siasa bila vitendo.

Prof Mwandosya ndie alielazimisha kujengwa uwanja wa ndege wa Songwe ima wahuni hawakupenda wakampeleka mtu agombee kwenye ujumbe wa NEC ili kumtoa Prof kwa bahati nzuri alishinda kwa kura chache sana Mbeya hawajui wanataka nini wao wapo busy na Siasa mbovu hata kwa madhara ya Mkoa wao wao wanaona sawa tu.