Halmashauri ya Jiji Mwanza ikiongozwa na Mkurugenzi, haitoi ushirikiano kwa Waandishi wa Habari

Halmashauri ya Jiji Mwanza ikiongozwa na Mkurugenzi, haitoi ushirikiano kwa Waandishi wa Habari

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Mimi ni mmoja wa Waandishi wa Habari wa hapa Mwanza, kero yangu ni kuhusu Mamlaka za Halmashauri za Jiji kutotupa ushirikiano baadhi ya Waandishi wa Habari tunapohitaji taarifa mbalimbali hasa hasa takwimu na zile zinazohusu miradi iliyotumia pesa kutoka Ofisi za Jiji.

Kumekuwa na danadana nyingi kutoka kwa Mkurugenzi wa jiji hilo (Kiomoni Kibamba) kwani amekuwa akizungusha waandishi kwa zaidi ya miezi miwili sasa.

Kila tunapomtafuta kwa ajili ya kupata ushirikiano wake amekuwa akituahidi tufike ofisini kwake na kila tunapofika huwa haonekani na kila anapotafutwa anaeleza kuwa atafika kitu kinachotufanya waandishi kumsubiri kwa muda mrefu bila mafanikio kwani huwa hafiki kabisa.

Aidha, Mkurugenzi huyo amekuwa akikata simu au kuzima simu kabisa pale anapoona kuwa ametudanganya vya kutosha waandishi.

Imekuwa ni tabia yake pale ambapo anapohitajika yeye mwenyewe kutolea ufafanuzi jambo fulani bali amekuwa akiwaelekeza Waandishi wawatafute Watu wa chini yake ambao pia wakifikiwa hukana taarifa hizo na wamekuwa wakieleza kuwa hawajapokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi.

Hali imekuwa ituwafanya Waandishi kushindwa kufanya kazi zao kwa kukosa taarifa kutoka kwenye mamlaka kwani mara nyingi habari hizo huhitaji upande wa pili wa mamlaka, hasa hasa habari zinazohitaji takwimu na miradi iliyotumia pesa.

Natoa wito Mamlaka hizo mkoani mwanza zibadilike ili kuwapa nafasi nzuri waandishi kufanya kazi zao kwa wakati.
 
Mwandikeni vibaya ili anitokeze akanushr kuwa yeye siyo fisadi.

Andikeni habari iliyooegemea upande mmoja
 
Back
Top Bottom