DOKEZO Halmashauri ya Kigamboni inakata pesa ya TALGWU bila idhini ya mwajiriwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwajiriwa wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wananikata TALGWU tokea nimeajiriwa bila kushirikishwa na bila kuandika jina la kujiunga na bila kutia sahihi yangu sehemu yoyote

Nimefika Halmashauri kwa Maafisa Utumishi majibu yao sio mazuri wananiambia kuwa ni lazima kujiunga na hiki chama cha TALGWU wakati sio lazima kujiunga, na ukitaka wakutoe wanakataa wanasema ni lazima

Ajira mpya wamekatwa TALGWU bila idhini yao na pia hawajasign form yoyote ile wakiwafuata afisa utumishi wanajibiwa majibu ya ovyo kuwa wasumbufu

Tunaomba TAKUKURU iingilie kati sababu pesa zinakatwa bila idhini ya waajiriwa wa KIGAMBONI.

#TAKUKURU #UWAJIBIKAJI #KIGAMBONI #TALGWU #AFISAUTUMISHI #WIZI #RUSHWA #UOVU
 
Hili tatizo na mimi limenikuta naona hawa TALGWU wanafanya uhuni usio na maana tatzo tukitoa malalamiko hatusikilizwi chama chenyewe cha kihuni tu hakina faida yoyote
 
Poleni sana ngoja wataalam waje na majibu. Mnakatwa shilingi ngapi?
 
Mimi ni mwajiriwa wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wananikata TALGWU tokea nimeajiriwa bila kushirikishwa na bila kuandika jina la kujiunga na bila kutia sahihi yangu sehemu yoyote

Nimefika Halmashauri kwa Maafisa Utumishi majibu yao sio mazuri wananiambia kuwa ni lazima kujiunga na hiki chama cha TALGWU wakati sio lazima kujiunga, na ukitaka wakutoe wanakataa wanasema ni lazima

Ajira mpya wamekatwa TALGWU bila idhini yao na pia hawajasign form yoyote ile wakiwafuata afisa utumishi wanajibiwa majibu ya ovyo kuwa wasumbufu

Tunaomba TAKUKURU iingilie kati sababu pesa zinakatwa bila idhini ya waajiriwa wa KIGAMBONI.

#TAKUKURU #UWAJIBIKAJI #KIGAMBONI #TALGWU #AFISAUTUMISHI #WIZI #RUSHWA #UOVU
Sheria ya kazi na mahusiano kazini, inakutaka uwe na chama, kama hujajaza form maana yake si mwanachama ila sheria inakutaka ukatwe pesa ya kuchangia ktk chama cha wafanyakzi, muhimu kwako kachukue fomu ili uwe mwanachama halali uwwze kupata haki zako kama mwanachama, kwani kutojaza fomu kunakunyima haki ya kuhudumiwa na chama chako
 
Si kweli.
Mimi huu mwaka wa 10 kwenye utumishi wa umma sikatwi kwenye mfuko wowote wa chama cha wafanyakazi.
Huko Halmashauri pasua kichwa watu wanaongoza watumishi utadhani wanaongoza ng'ombe .
Local government watumishi wapya kabla ya mifuko kuunganishwa ma HR walikuwa wanawachagulia mfuko watumishi sometimes mpaka aina ya benki ya kupitishia mshahara. Wakipewa katakrima kidogo tu mtumishi unapelekwa watakavyo wao
Screenshot_20250310-151423.jpg
 
Back
Top Bottom