Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ina mzunguko mkubwa wa pesa ila ina miundombinu mibovu sana

Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ina mzunguko mkubwa wa pesa ila ina miundombinu mibovu sana

kahembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Posts
227
Reaction score
310
Mitaa ya Majego, Nyasubi, Nyamhongolo, Nyihogo, Phantom, Nyakato, Mbulu, Marunga, Zongomela, Dodoma viwandani. Hiyo ni baadhi ya mitaa ya mjini ila hakuna sehemu hata Moja yenye Barabara ya lami. Barabara zote ni za vumbi sijui madiwa na Mh. Mkurugenzi hamlioni hilo.

005caeb3196e4e9889be731a7289fdb0.jpg
 
Mitaa ya Majego, Nyasubi, Nyamhongolo, Nyihogo, Phantom, Nyakato, Mbulu, Marunga, Zongomela, Dodoma viwandani.. hiyo ni baadhi ya mitaa ya mjini ila hakuna sehemu hata Moja yenye Barabara ya lami...Barabara zote ni za vumbi sijui madiwa na Mh. Mkurugenzi hamlioni ilo

Kwani ungependa wenye meno wakale wapi?
 
Wasiichague tena CCM.

Kwani uliambiwa huwa wanaichagua?

"Au Kwani safari hii wakipigia wale wa ule upande mwingine sasa ndiyo watatangazwa washindi?"

Kwani aliyeyasema hayo alishaacha kugombea?
 
Changamoto sana

Pana habari za mkurugenzi wa halmashauri hapo kukaa ofisini tangia kipindi cha msoga hadi juzi kati ya Samia hapa.

Ya nini kumung'unya Maneno:

"Barabara ngapi za manispaa hiyo yenye hadhi ya Shinyanga, Moshi au Morogoro zitakuwa zimeendelea kujengwa matumboni mwa wakubwa tena walio wazito kweri kweri katika kipindi chote?"
 
Watu wanakandamiza tu kizenji, ripoti ya CAG ikija na madudu hakuna hatua inayochukuliwa, ndio mfumo ambao tanzania imejijengea, yani upigaji ni sumu iliyosambaa kote, mtu imefikia hatua rushwa ama upigaji anaona ni haki yake.
 
Utakuta wachapaji ni wengi hapo halmashauri.

Kwamba kama manispaa Kahama ni sawa na Moshi, Morogoro, Shinyanga, nk?!

Kahama ukweni huko nimetembezwa nikaonyeshwa yalipokuwa makazi ya aliyekuwa waziri wa ulinzi kipindi cha jiwe marehemu "Elias Kuandikwa:"

Nyumba nzuri kwenye fence nzuri. Barabara iliyopewa jina lake kuelekea hapo: "aibu!"

Hadi kibao chenye jina lake wamekitoa na kubakia nguzo ya njano na weusi inayoendelea kusimama kama ushahidi.

Ama kweli asiyekuwapo na lake halipo!
 
Watu wanakandamiza tu kizenji, ripoti ya CAG ikija na madudu hakuna hatua inayochukuliwa, ndio mfumo ambao tanzania imejijengea, yani upigaji ni sumu iliyosambaa kote, mtu imefikia hatua rushwa ama upigaji anaona ni haki yake.

Haipo shaka wakandamizaji hao watakuwa ni vigogo kweri kweri:

1. Kahama banks zilizopo ni nyingi kuliko zilizoko hadi kwenye majiji mengine hapa nchini.

2. Huko wana hadi ma KCB, Access na zingine sizikumbuku zenye majina tu ambazo sikupata kuzisikia kwingine, ila huko naliziona.

3. Banks huko zafunguka hadi jumapili, usiku na hata siku za sikukuu!

4. Yasemekana umekuwapo mkoa wa TRA huko tangia ikiwa halmashauri ya wilaya kabla ya jiwe.

5. Tanesco nao wana mkoa wao huko. Polisi sina uhakika.

6. Nk, nk.

Yote tisa, ila hiyo wilaya ni manispaa lakini si mkoa 🤣🤣.

Barabara ndiyo hizo?!

Wajameni! Mkandamiza kizenji atakuwa ni "kaj*mba" nani hapo?

Panga, pangua: Iko namna!
 
Kuna Bank zifuatazo. EXIM BANK, DTB, ACCESS BANK, AZANIA BANK, POSTA BANK, +NMB, CRDB, NBC BANK
 
Back
Top Bottom