Halmashauri ya mji wa Bunda yashindwa kutoa Tsh. 275,000 kuvuta maji shule msingi Nyabehu

Halmashauri ya mji wa Bunda yashindwa kutoa Tsh. 275,000 kuvuta maji shule msingi Nyabehu

danieltz

Member
Joined
Feb 18, 2022
Posts
28
Reaction score
39
Katika kuzurura kwangu nikakatiza Halmashauri ya mji wa Bunda kata ya Guta kijiji cha Nyabehu katika shule ya msingi Nyabehu, Aibu niliyokutana nayo katika shule hii ni aibu mbaya kwa Halmashauri ya mji ya Bunda, kwenye shule hii tangu kuanzishwa kwake hakuna huduma ya maji hali inayopelekea wanafunzi kujisaidia bila kunawa na vyoo kuwa vichafu mda wote.

Tangu kuanzishwa kwa shule hii wakuu wa shule wamekuwa wakituma maombi Halmashauri kuvutiwa maji kuondoa kero hii lakini wamekuwa wakizungushwa miaka na miaka, aibu ni kwamba gharama za kuvuta maji ambazo mkuu wa shule alinidokezea zilikuwa ni 275000 tu pamoja na vifaa Nikajiuliza hivi kweli Halmashauri inashindwa kuidhinisha laki 2 na elfu 75 kuvuta maji, wanafunzi wamekuwa wakipata shida mnoo wengine uja na maji yao toka nyumbani wengine hununua kwenye mabomba ya mtaani.

Shule ililazimika kuwaambiwa wazazi wachange kila mwezi kiasi cha Tsh 1000 ili kununua maji kwa matumizi ya kila siku lakini bado muitikio ni mdogo kwa wazazi kutoa kiasi hiko cha fedha, Shuke ilipata mfadhili kupitia mradi wa USDA na wakajengewa tanki la maji lenye uwezo wa kubebea zaidi ya lita 10000 lakini cha kusikitisha hakuna chanzo cha maji hivo tenki hilo limekuwa kama urembo shuleni hapo wakati mwingine ni kusubiri kipindi cha masika kuvuna maji ya mvua.

Bado najiuliza Serikali inakosaje laki 2 ya kuvutia maji. Tunaomba Serikali na Halmashauri ya mji wa Bunda ihakikishe shule ya nyabehu inapata maji mara moja kupekuka kero wanazo kutana nazo wanafunzi wa shule hiyo.

KUHUSU FEDHA ZA RUZUKU

Niliendelea kudodosa kujua fedha za rukuzu zinavyotumika kama zingeweza kutumika kuvuta maji hapo nako nilikutana na aibu nyingine nzito, Ni kwamba kwa mwezi wanapokea fedha za ruzuku kiasi cha Tsh 104000/= laki moja na elfu nne tu kwa ajili ya matumizi ya shule fedha ambazo ni kiduchu kwani kutoka tu kijiji cha nyabehu hadi bunda mjini nauli tu ni 12000 na kipindi cha masika ni 20000 yani ukipewa hiyo hela ya rukuzu ukanunue mahitaji mfano chaki basi uhakikishe unaenda kwa nauli yako. Pia fedha hiyo ya rukuzu ndo itumike kuandaa mitihani ya muhula yani laki moja uchape na kuprint na kutoa copy kwa wanafunzi 240 kwa masomo saba.

Imefika hatua walimu wamekuwa wakitoa fedha zao mfukoni ili mambo yaende mbaya zaidi wakaguzi wakija hawajali kusikiliza kero za hapo shuleni wakifika hapo ni kukaripia tu na kuondoka.Serikali na Halmashauri ya Bunda ione aibu kwa mambo madogo na ya muhimu kama haya.

DED wa Bunda mji ahakikishe shule ya nyabehu inapata maji kwani Maji ni uhai wanafunzi wanapata shida mnoo.

Sitaki kusema kwamba Halmashauri imekosa laki 2 hapana serikali haiwezi kosa laki mbili najua wanazo kuondokoana na aibu hii wahakikishe manaweka maji shuleni hapo.


WENU
MFUKUNYUKU
IMG_20240901_114838_297.jpg
IMG_20240901_114733_463.jpg
 
Wanafunzi hiyo shule ya Nyabehu wanaenda sana chooni inavyoonekana kwa mjibu wa mleta mada

Hivi hao wanafunzi wanaenda shuleni kusoma au kwenda chooni?
 
Kwhy hoja yako nini kwamba wasijisaidie au Wasipewe maji kisa wanaenda sana chooni?
 
Kwhy hoja yako nini kwamba wasijisaidie au Wasipewe maji kisa wanaenda sana chooni?
 
Back
Top Bottom