A
Anonymous
Guest
Kumekuwepo na sintofahamu kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi za Serikali kutokana na utaratibu mbovu katika kugawa vitabu vya shule za msingi kwenye Halmashauri yetu ya Momba.
Vitabu vinarundikwa katika Ofisi za Halmashauri ya Momba na Maafisa kutoka Idara ya Elimu Msingi kuwaagiza Walimu Wakuu kufuata vitabu hivyo Ofisi za Halmashauri kwa kutembea umbali mrefu sana na kwa kutumia gharama kubwa.
Lakini pia hali hii imesababisha baadhi ya shule kutopata vitabu kwa uwiano sahihi kutokana na vitabu kutelekezwa na Walimu Wakuu, baadhi yao wanachukua bila utaratibu na baadhi ya vitabu kuharibika kwa kulowa kutokana na mvua zinazoendelea.
Tunaiomba Halmashauri isaidie kusambaza vitabu hivyo hata angalau kuvifikisha katika Kata ili kuepusha usumbufu mkubwa kwa Walimu Wakuu hao wanaoteseka kusafirisha vitabu umbali mrefu ikiwa Halmashauri ina Magari ya kutosha kusambaza vitabu hivyo vilivyofika Mwezi huu Januari 2025.