Halmashauri ya Ubungo yafafanua madai ya maeneo ya Mbezi Luis na Magufuli Terminal kunuka harufu ya mikojo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876


Hoja ilipoanzia ~ Maeneo ya Stendi ya Mbezi Maramba, Darajani, korido la jengo la Abiria na Gereji (Stendi ya Magufuli) kunanuka mikojo
TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU UFAFANUZI WA TAARIFA YA HARUFU YA MIKOJO KATIKA MAENEO YA STENDI YA MALAMBA, DARAJANI, KORIDO ZA JENGO LA ABIRIA NA GEREJI YA STENDI YA MAGUFULI

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii, hususani taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa kijamii wa JamiiForums tarehe 10 Septemba 2026, yenye kichwa cha habari: "Maeneo ya Stendi ya Malamba (Mbezi), Darajani, Korido za Jengo la Abiria na Gereji (Stendi ya Magufuli) Kunuka Mikojo."

Kufuatia taarifa hiyo, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inapenda kuujulisha umma kwamba hakuna harufu ya mikojo katika Jengo la Abiria wala katika eneo la Gereji lililopo katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli, kama ilivyoelezwa katika taarifa hiyo.

Halmashauri inaendelea kutekeleza majukumu yake ya usimamizi wa Kituo hicho pamoja na miundombinu inayozunguka kituo hicho, kwa kuhakikisha kuwa mazingira yanaendelea kuwa safi na salama wakati wote. Usafi katika kituo hicho hufanyika saa 24, sambamba na kuchukua hatua stahiki dhidi ya watu wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za usafi na utunzaji wa mazingira.

Aidha, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inaendelea kuwasisitiza wananchi na watumiaji wote wa kituo hicho, pamoja na watumiaji wa miundombinu inayozunguka kituo, kushirikiana katika kulinda na kutunza mazingira kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usafi na utunzaji wa mazingira ndani na nje ya kituo.

Hata hivyo, kwa maeneo ya Darajani na Stendi ya Malamba, Halmashauri inaendelea kufuatilia hali ya usafi katika maeneo hayo ili kubaini kama kuna changamoto hiyo na, endapo itabainika kuwepo, hatua stahiki za usafi zitafanyika ili kutunza mazingira.

Halmashauri inasisitiza kuwa utunzaji wa mazingira ni jukumu letu sote.

Imetolewa na:

IMETOLEWA NA: KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
 
ZILE SMS ZA TUNZA AMANI TULIZIONA ,SASA TUNATAKA SMS ZA ELNINO KWENYE SIMU ZETU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…