Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya kuuza kwa Shule ya Msingi Ubungo National Housing hivi karibuni, Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imekanusha uvumi unaoenea mitandaoni kuhusu kuuzwa kwa shule hiyo.
Taarifa hiyo imewataka wazazi kutokuwa na hofu, kwani shule hiyo ipo katika ukarabati mkubwa unaoendelea tangu Julai 11, 2024, kwa lengo la kuboresha miundombinu.
Soma Pia: Taharuki yazuka, Wazazi wajaa Shule ya Msingi Ubungo NHC baada ya taarifa kuwa shule inauzwa
Aidha taairfa hiyo ilidokeza kuwa umati wa wazazi uliokuwepo shuleni hapo ulikuwa ni kwa lengo la kuandaa kikao cha shule ambacho kiliahirishwa kutokana na Mwalimu Mkuu kupata changamoto ya kiafya
================================================
Kumetokea taarifa iliyosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikionyesha wazazi wakikusanyika katika Shule ya Msingi Ubungo National Housing na kueleza kuwa shule hiyo imeuzwa na kwamba wazazi wameambiwa wakawachukue watoto wao wakawatafutie shule.
Kufuatia taharuki hiyo iliyojitokeza, mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo anapenda kuwataarifu wananchi hususan wazazi wenye watoto katika shule hiyo kuwa taarifa hizo si za kweli na zinalenga kuleta taharuki katika jamii.
Ukweli ni kwamba;
1. Shule hiyo ipo katika mkakati mkubwa wa ukarabati na ilipangwa kuwa ya mfumo wa Kiingereza. Ukarabati ulianza toka Julai 11, 2024 ambapo unahusisha ujenzi wa madarasa manne ambayo yamefikia katika hatua ya renta.
Mpango huo mkubwa wa ukarabati hauathiri wanafunzi wanaosoma kwa sasa, isipokuwa mkuu wa shule aliitisha kikao cha wazazi jana tarehe Novemba 11, 2024 ili kikao kifanyike leo Novemba 12, 2024 kuwaeleza juu ya mpango huo wa uboreshaji wa shule hiyo. Kikao hicho hakikufanyika kutokana na changamoto za kiafya za mkuu wa shule.
2. Wakati wa ukarabati wa shule, mara nyingi huwa tunakuwa makini sana na watoto. Ikionekana ni ukarabati mkubwa au ujenzi mpya, huwa tunahamisha watoto kwenda shule za karibu na baadaye kurejea. Kwa hiyo, mpango wa kuhamisha watoto ulikuwa bado haujaanza.
3. Tutafanya kikao na wazazi wenye watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Ubungo NHC ambao ndio wadau wa elimu kwenye ngazi ya msingi ili kupata picha ya pamoja ya mikakati mikubwa ya kuboresha shule hiyo na kukubaliana mfumo mpya wa shule, kwa sababu wazazi wana nafasi ya kutoa maoni yao.
Aidha, tunatoa onyo kwa mtu au kikundi chochote kinachovumisha taarifa zinazoletea taharuki hasa kipindi hiki kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mwisho, tunawakumbusha kuwa kusambaza taarifa za uongo na zisizo sahihi ni kosa kisheria. Unapokutana na habari kama hizo ambazo hazina uhakika ni vyema kuwasiliana na mamlaka husika ili kupata ufafanuzi na taarifa sahihi.