Mimi ni mwalimu, nahitaji TSD number, nimeenda halmashauri ya wilaya yangu Mkalama kufuatilia lakini bahati mbaya hiyo huduma haipo. Nimemwuliza DEO lakini kaniambia hizo TSD number tutatafutiwa tu halafu tutapewa!... Sijaridhika na jibu la mkuu wangu wa idara maana mie nina miezi 4 kazini, na ninastahili kuipata ndo maana naitafuta kwa makusudi fulani. Hivyo kwa mwenye kujua anisaidie ni wapi ntaipata.