Halmashauri ya (W) Mkalama haina ofisi ya T.S.D (teachers service department), niipate wapi?

SuperSami

Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
30
Reaction score
2
Mimi ni mwalimu, nahitaji TSD number, nimeenda halmashauri ya wilaya yangu Mkalama kufuatilia lakini bahati mbaya hiyo huduma haipo. Nimemwuliza DEO lakini kaniambia hizo TSD number tutatafutiwa tu halafu tutapewa!... Sijaridhika na jibu la mkuu wangu wa idara maana mie nina miezi 4 kazini, na ninastahili kuipata ndo maana naitafuta kwa makusudi fulani. Hivyo kwa mwenye kujua anisaidie ni wapi ntaipata.
 
Hiyo ndo changamoto ya wilaya mpya!!! Usishangae kuona afisa elimu hajui hata TSD ina umuhimu gani kwa kazi ya ualimu. So kama hajui ina kazi gani kwa ninyi mliochini ya idara hiyo mna hasara! Maana hata hupati mkopo NMB bila TSD number/letter, huwezi kuhama kama huna TSD number na pia hupati haki zingine za ki maslahi bila TSD number.
Nawapa pole walimu mlio halmashauri mpya hususani ninyi wa Mkalama. Lakini pia ni aibu kwa idara ya utumishi pamoja elimu.....' Nikipata nauri nitakuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…