DOKEZO Halmashauri ya Wilaya Mvomero haijaanza kutoka mikopo ya 10% licha ya kutakiwa kutolewa kabla ya Novemba 30

DOKEZO Halmashauri ya Wilaya Mvomero haijaanza kutoka mikopo ya 10% licha ya kutakiwa kutolewa kabla ya Novemba 30

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Wami Dakawa, Wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro

Lalamiko langu kwa Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Mvomero na Mkurugenzi Mtendaji kwani hadi sasa hatujapata mrejesho wa maombi ya mikopo inayotokana na mapato ya Asilimia 10 ya Halmashauri ambayo inalenga kuinua uchumi kwa makundi maalumu kama vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

Kupitia mtandao wa WhatsApp ukurasa wa TAMISEMI kuna taarifa ya MIKOPO YA ASILIMIA 10 KUANZA KUTOLEWA KABLA NOVEMBA 30, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt Festo Dugange alisema mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10 itokanayo na mapato ya ndani ya Halmashauri kwaajili ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inatarajiwa kuanza kutolewa kabla au ifikapo Novemba 30, 2024 ili kuweza kuwanufaisha walengwa wa mikopo hiyo.

Mhe. Dkt Dugange amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mheshimiwa Santiel Eric Kirumba Mbunge wa Viti Maalum aliyeuliza Je, lini Serikali itarudisha mikopo ya asilimia 10 kwa Makundi Maalum.?

Lakini cha kushangaza Leo tarehe 25 decemba 2024 , vikundi vingi hatujapata mrejesho wowote wala kusikia kuwa kuna watu wamepatiwa fedha hizo na ukizingatia vikundi vingi tulifanya jitihada ya kupata mikopo hiyo kwani tumetumia pesa nyingi ili kukidhi vigezo vya usajili lakini mwisho tunajilaumu bora tungetumia pesa zile kwenye mambo mengine ya kijasiriamali

Kila tukiingia kwenye mfumo Notification inatuonyesha NEXT APPROVER ni (DCDO) ,Kiukweli tushakata tamaa ila bora ukweli usemwe

Pia soma > Mikopo ya Asilimia 10 Kuanza Kutolewa Kabla ya 30 Novemba, 2024.

Screenshot_20241225_122122_Chrome.jpg
Screenshot_20241225_114848_Chrome.jpg
Screenshot_20241225_114906_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom