KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Mimi ni Mtumishi wa Serikali hapa Mpwapwa Mkoani Dodoma, kero moja kubwa ni kuwa kuna urasimu wa upandishwaji wa Madaraja ya Mishahara na pia baadhi ya wenzetu lugha mbaya wanapokuwa katika majukumu yao.
Kinachouma zaidi ni kuwa kuna watushi wana miaka zaidi ya kumi hawajapandishwa licha ya kuwa utendaji kazi wao ni mzuri, viongozi wa Mpwapwa wanapoulizwa wanasema tatizo lipo Utumishi Makao Makuu wakati uhalisia ni kuwa tunajua baadhi ya Watu walioshika nafasi zenye mamlaka ndio sababu.
Gharama za maisha zinazidi kubadilika kwa kupanda kila mwaka lakini pato letu limebaki vilevile wengi wetu, hiyo inatutoa katika mstari wa kutimiza majukumu yetu kwa ufanisi.
Viongozi wetu tunaowauliza kulikoni wanadai wameshatuma barua katika ngazi za juu lakini tatizo lipo katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyomo kwenye barua.
Kutokana na hali hiyo, kinachoendelea kinatengeneza mazingira ya rushwa na ile kujuana, kwa ufupi ni upendeleo.
Nimeamua kutumia nafasi hii ya JF kwa kuwa Watu wanaogopa kusema kwa kuwa ukitumia nguvu nyingi kusema au kuhoji unaonekana ni Mwanasiasa au mwanaharakati.