Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA YATOA MIKOPO YA THAMANI YA SHILINGI MILIONI MIA NNE (Tsh 400m)
Jana, Ijumaa, tarehe 3 Jan 2025, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) ilitoa mikopo isiyokuwa na riba ya kiasi cha Tsh Milioni 400 (Tsh 400m) kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Mgeni Rasmi kwenye tukio hilo muhimu sana alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma (DC), Mhe Juma Issa Chikoka
Viongozi mbalimbali, akiwemo Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, walihudhuria hafla hiyo.
CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa: Tafadhali sikiliza ushauri na nasaa mbalimbali zilizotolewa kwenye hafla hiyo iliyofanyika Kijijini Suguti, Makao Makuu ya Halmashauri yetu.
Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6, Musoma
Tarehe: Jumamosi, 4 Jan 2025