DOKEZO Halmashauri zijitathmini sana juu ya kuwatumia mawakala kukusanya mapato

DOKEZO Halmashauri zijitathmini sana juu ya kuwatumia mawakala kukusanya mapato

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Hawa mawakala wanaoingia mkataba na Halmashauri za Wilaya kukusanya mapato wanawapunja sana hizi Halmashauri na Halmashauri zinatakiwa zijitathmini sana.

Nitoe mfano ulio hai hapa Mwanza. kuhusu ushuru wa madini.

(1) Kwa wastani kwa siku kuna malori 50 yanayosomba mchanga.

(2) Kila lori kwa siku inafanya tripu 4

(3) Hivyo kwa siku kwa malori 50 ni tripu 200.

(4) Kwa tripu moja kila lori linalipa Tshs.10,500 japo ni ghali sana.

(5) Kwa siku fedha inayolipawa kwa wakala ni Tripu tripu 200 x 10,500 = T.shs.2,100,000.

(6) Kwa mwezi fedha anayokusana wakala ni T.shs. 2,100,000 x 30 = T.shs.63,000,000.

(6) Fedha nayokusanya wakala kwa mwaka ni T.shs. 63,000,000 x 12 = T.shs.756,000,000.

Hiki ni chanzo kimoja tu. Sijui wakala anawasilisha kiasi gani kwenye Halmashauri. Fanyeni utafiti kwa kweli kutumia mawakala kunawapunja sana Halmashauri kimapato.
 
Back
Top Bottom