Halmashauri zote zatakiwa kusimamia uondoaji wa takataka kwenye masoko ili kulinda afya za Watu

Halmashauri zote zatakiwa kusimamia uondoaji wa takataka kwenye masoko ili kulinda afya za Watu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ummy Mwalimu amezielekeza halmashauri zote kuwa na miundombinu bora ya kukusanya, kuhifadhi na kusafirisha taka ili kulinda afya za wananchi.

Alitoa maelekezo hayo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Soko la Majengo jijini Dodoma kuangalia mfumo wa takataka ngumu.

Akiwa amefuatana na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Mazingira, Waziri Ummy, alionesha kuridhishwa na hali ya mazingira sokoni hapo na kuipongeza halmashauri ya jiji hilo.

Alizitaka halmashauri zote zitoe kandarasi za kukusanya na kusafirisha takataka kwa watu wenye vifaa bora kwa ajili ya kazi hiyo.

“Tumeona gari za kukusanya na kusafrisha taka zenyewe zikiwa ni takataka kwa hiyo tutakagua kila halmashauri wajitathmini je, kandarasi hii waliyompa mtu wa kukusanya, kuhifadhi na kusafirisha taka ana vifaa bora.”

“Hizi ni salamu tu tunataka masoko yawe safi na salama kwa wanaouza na wateja, kikubwa tunasema mazingira safi na salama kwa ajili ya maendeleo endelevu,”alisema Ummy.

Alisema utafanyika ukaguzi wa kuona kama wakandarasi hao wana vigezo na sifa zikiwemo kuwa na vifaa vya kuwakingia watumishi wanaokusanya takataka.

Alisisitiza uwepo utaratibu wa kuondoa takataka zinazokusanywa na kuhifadhiwa kwenye masoko kwa wakati na kwamba hatavumilia kuona halmashauri ambayo takataka zinakaa kwa zaidi ya siku moja.

Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 na kanuni zake inazitaka halmashauri zote za majiji, manispaa, miji na wilaya kuweka mifumo bora ya kukusanya, kuhifadhi na kusafirisha taka.

Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Takataka Ngumu jijini la Dodoma, Dickson Kimaro, alisema wana changamoto ya kupotea vifaa wanavyopewa vibarua na kuahidi kuendelea kutoa vifaa vifaa hivyo.
 
Back
Top Bottom