The MoNA
JF-Expert Member
- Sep 19, 2014
- 4,168
- 10,184
Ndugu wana Jamuhuri ya Muungano,
Kwa mnaotumia halotel limewakuta hili?
Wiki iliyopita mpaka hii tuliyopo kuna uhuni halotel wanaufanya. Unajiunga GB 1 ndani ya dakika 30-60 unapata na huu ujumbe;
Mpendwa mteja! Umemaliza kifurushi chako cha intaneti. Kuendelea kutumia intaneti jiunge tena kifurushi kwa kupiga *148*66#. Asante!
Hapo haujaingia instagram wala youtube ni hapa hapa JF na Whatsapp ambapo kote hamna auto download na hata video za whatsapp ndan ya dakika hizo haziwezi kumaliza mb zote. Nina matumizi madogo sana ya mb kwa kutwa.
Siku za nyuma GB 2 naweza kaa nazo hadi siku 3 ila kwa siku kadhaa hizi lisaa likipita ni kituko cha huo ujumbe.
Juzi ndio kituko mpaka nikawapigia simu mdada huyo akaniambia zima simu kisha uwashe ina maana wanajua wanachokifanya.
Mchana nilijiunga GB Saa 13:34 saa 14:48 kifurushi kimeisha na nilikua nina google tu. Sikuingia youtube wala instagram.
Hata ukijiunga vya 5000 utapeli ni huu huu.
Nafungia line yao kwa muda naenda TTCL huko vida tigo airtel nako majanga tu.
Sijui kama kuna mwingine analipitia hili kutoka Halotel?