KERO Halotel Tanzania boresheni huduma zenu

KERO Halotel Tanzania boresheni huduma zenu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Halotel Tanzania ina zaidi ya miaka 8 katika utoaji wa huduma ya mawasiliano nchini lakini inashangaza kuna mambo madogo madogo tu wanashindwa kuyaweka sawa ili kuiboresha huduma yao kimawasiliano

Jambo la kwanza ni namba kuwa busy pale unampompigia mtu wa halotel ukiwa na laini ya Halotel pia. Hapa utakuta simu unapiga husikii kuambiwa namba ya simu inatumika bali utaona tu simu inakata tu na kuandikiwa line busy. Hili limekaa katika mfumo kama vile mtu anakukatia simu kimakusudi kabisa, tofauti na mitandaoni mingine ukimpigia mtu simu utajulishwa kabisa kwa ujumbe wa sauti kuwa mteja unayempigia anaongea na mtu mwingine tafadhari jaribu tena baadae.

Jambo la pili ni call waiting. Ukiseti call waiting, mtu akikupigia wala hajulishwi kuwa mteja unayempigia anaongea na simu nyingine tafadhari subiri au jaribu tena baadae, bali huyo mtu atasikia tu simu inaita kama kawaida tu mteja anayepiga hapewi ujumbe wa sauti wala wa maandishi.

Jambo la tatu ni conference call. Sijui inakuaje mpaka leo hii limekuwa jambo gumu kwa Halotel watu kufanya mazungumzo kwa kuunganishana. Call conference ina faida yake kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya pamoja n.k lakini hadi leo hii halotel wameshindwa kuweka hii huduma kwenye mifumo yao.

Kwangu ni hayo, wengine watasema mapungufu mengineyo ili iboreshwe.
 
Waboreshe huduma haswa, code ya CRDB *150*03# kwa halotel kuna muda ni changamoto kubwa sana... Unakuta mtu unataka kutuma pesa ya dharula tena kwa haraka lakini hakuna mafanikio
 
Na halopesa app huwezi itumia mpaka utumie internet ya halotel. Nilishangaa sana, kwa sababu mpesa app huwa naitumia tu hata nikiwa na internet ya mtandao mwingine.
 
Back
Top Bottom