Hama hama ya watangazaji wa radio za Bongo, maana yake ni nini!?

Hii inamaanisha "fursa" vijana wasomee uandishi, utangazaji na Udj. Soko liko wazi
Ni kweli hii ni fursa ya watangazaji na waandishi wa habari kujiongeza na kuongeza ubunifu ili kupata mikataba yenye maslahi manono. Hivi sasa soko limebadilika na lina ushindani mkubwa hivyo kuhitaji njia mbadala ili kuweza kulifikia na kuliteka. Kuna watangazaji na waandishi wengi ambao wamezoea kufanya kazi kwa mazoea hii itawafanya waongeze bidii.
 
Its too much nasema inatosha IPP MEDIA MKOJE??? Mliniondolea dj Mafuvu leo Dj Sinyiorita .... Badiliken bana mnatukwaza mashabiki wenu aghhhhhhhh
IPP MEDIA ni kama Arsenal na wenger wao ni m'bahili kusajiri.
 
Watangazaji wengi wanafanya kazi kwa mazoea lakini wanategemea kulipwa zaidi!
 
Watangazaji wengi wanafanya kazi kwa mazoea lakini wanategemea kulipwa zaidi!
Kama wakiendelea kubaki na hiyo dhana muda sio mrefu watajikuta wako nje ya soko la ajira ya watangazaji na waandishi wa habari. Hebu wajifunze kwa wenzetu wa nchi jirani walivyo. Yaani huwa nafurahi sana jinsi hawa watangazaji wa Knya wanavyojipanga na wanavyojitahidi kuwa wabunifu.
Kwa mfano angalia taarifa za habari za wenzetu huwa zinachukua zaidi ya masaa mawili na yote hayo ni kuhakikisha hawaachi ombwe kwa msikilizaji. Kukiwa na mada inavyodadavuliwa kitaalamu utapenda kusikiliza na kuwaangalia wanavyotumia utaalamu wao. Pia jinsi watangazaji wanavyojiandaa kufanya mahojiano, maswali huwa yanalenga kwenye uchonozi wa taarifa hapo utaona tofauti kubwa sana na watangazaji wetu.
Lingine kubwa ni mandhari ya studio zao zinapendeza saana. Zina na kila ya mbwembwe ambayo haichushi macho ya mtazamaji. Nafikiri ndio maana watangazaji kama Tido Mhando na Charles Hilary wameliona hilo, ila kuna sehemu naona kama hawako huru sana kama kawaida yao. Hawafunguki kama kawaida yao. Ule uwezo wao wa kuhoji hauonekani kutumika ipasavyo kama walivyokuwa kwenye vyombo vya habari vya nje ya nchi. Wamepwayaaa, kulikoni?
 
Watangazaji wetu wengi mind set yao ni kulipwa sana wakati ubunifu zero...mtu anataka alipwe sana wakati hana ubunifu wa kuleta matangazo kwenye kipindi!
 
Watangazaji wetu wengi mind set yao ni kulipwa sana wakati ubunifu zero...mtu anataka alipwe sana wakati hana ubunifu wa kuleta matangazo kwenye kipindi!
Kwa hiyo matangazaji mwenye 'network' ya matangazo ndo anakuwa dili. Wape pole saana, watazamaji na wasikilizaji wa sasa wako tofauti. Wanataka radha na ubunifu.
Ukumbuke unaweza ukawa na matangazo mengi lakini hayana watazamaji au wasikilizaji, sijui huyo mwenye matangazo yake ataweza kupata kile alichokuwa anahitaji!
 
Biashara ya Radio na TV ni matangazo na lazima mtangaziji ahakikishe ana vuta watazamaji au wasikilizaji wengi na hapo ndio sponsor wanapatikana...na hakuna atakaye weza kukulipa zaidi ikiwa hauzalishi chochote.....
 
ninachokiona hapa ni kukomoana kati ya EFM na clouds. EFM ni threat kubwa kwa Clouds. Ruge kwa gharama yoyote ile atachukua watangazaji wazuri wa EFM ili kuimaliza. lakini kila mtu amepangiwa riziki yake. watakuja wazuri tu maana hata hao waliopo hawakujua kama watawapata.
 
Hivi Twalib Omary Muwa amehamia clouds kutoka Azam tv,maana nasikia leo sauti yake spotiextra ya clouds.Bora kidogo kipindi kitachangamka kilishaanza kupoa
 
Kuna dj ommycrayz yaan huwa simuelewi kabisa
Uko sawa na mm m mwenyewe huwa simuelewi anachokifanya.kifupi ea radio dj tegemeo kwa sasa n dj summer.Wakifanya makosa kumpoteza na huyo radio yao itapwaya mno
 


Zaidi ya Maulid Kitenge na Fredwaaaa, hakuna watangazaji wazuri hapa. Gardner hana sifa zozote za utangazaji na hajuwi tu kutangaza Zaidi ya kusifia ujinga na kuongea pumba. Wache hizo redio zitambiane ila wanajisumbua tu kuwapa watu ujiko wasio stahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…