Hamad Chande: Bajeti Zitazingatia Jinsia

Hamad Chande: Bajeti Zitazingatia Jinsia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. HAMAD CHANDE (NAIBU WAZIRI FEDHA) - BAJETI ZITAZINGATIA JINSIA

Serikali imeeleza kuwa Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2023/24 umetoa maelekezo kwa Maafisa Masuuli kuzingatia masuala ya Jinsia, wakati wa uandaaji, uwasilishaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini pamoja na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mpango na Bajeti zao.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande amesema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Halima James Mdee aliyetaka kujua muda ambao Serikali itaanza kutengeneza bajeti kwa jicho la jinsia.

Chande amesema pamoja na maelekezo hayo, Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake - UN Women, inaendelea kushirikiana na Serikali kujenga uwezo katika maandalizi ya nyaraka za sera kwa kuzingatia masuala ya kijinsia.

Alisema katika mwaka 2022/23, Wizara ya Fedha na Mipango imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kuboresha Mwongozo wa maandalizi ya mipango na bajeti ya Serikali kwa jicho la kijinsia.

FvLriFJWYAIM_dL.jpg
 
Back
Top Bottom