Hamad Rashid Mohammed naye kuondoka CUF!

Nilisha sema huko nyuma kwanba hakuna wapnzani isipokuwa watu wana malengo yao lakini Hamadi Rashidi hawezi kwenda Chadema kwa kuwa wapenba wana ubaguzi wa dini na ukabila maana wao wanajifanya ni waarabu
 
Hata ikiwa ni tetesi. Mimi nampongeza Bw. Hamad Rashid kama atachukua hatua hiyo. Anaweza kuwa kiongozi wa "the alternative Party" na tukaiendeleza Zanzibar (ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) . Ni Mwanasiasa mahiri sana huyo!

Hicho chama atakachoanzisha mfadhili wake mkuu atakuwa RA maana tayari huyu jamaa alishaonyesha kuwa kibaraka wa RA (kumbuka reaction yake kwa Mengi wakati wa issue ya mafisadi papa). Na kama atataka kujiunga vyama vingine, chama kama CHADEMA wasimkubali maana atakwenda kuwamaliza. Labda aende huko CCM kwa RA wake.
 
Last edited:
Karibu sana kwenye chama cha maendeleo na demokrasia mheshimiwa hamad rashid.njoo ukajiunge na wanaharakati wenzako wenye hari na bidii ya kunyoosha maisha ya watanzania kama wewe.
 
Huyo ni tawi la CCM ndani ya chama cha upinzani
 
Kuna kipindi RTD kinaitwa "mazungumzo baada ya habari". If wishes were horses, beggars would ride. Ndoto muanaota.Nani aende CCM?.
 

Alichouliza HAMAD RASHID ni sahihi kabisa kama Mengi alikuwa na ushahidi wa hujuma za Mapapa angezipeleka kwenye vyombo stahiki.hivi wewe umewahi kumuona mmiliki wa CNN akitumia CNN kuwasakama wenzake? hata muuaji ana haki zake kama Mfungwa n.k.

Hamad RASHID alimkosoa waziri mkuu aliposema kuwa atakayeua ALBINO naye auliwe.yeye PINDA kama nani anawahukumu watu wakati vyombo vya sheria vipo?HAMAD RASHID ni katika wabunge makini bungeni na mwenye uwezo mkubwa kisiasa.Nyerere alikuwa akimtegemea sana HAMAD RASHID na kumpenda sana kwa uwezo wake wa siasa.Slaa hana hata nusu ya uwezo wa HAMAD RASHID.

HUYU jamaa siasa iko kwenye Damu yake na elewa kuwa wanasiasa hasa wa PEMBA kwao rushwa ni adui namba moja,hata viongozi wanaotokea ZNZ mara nyingi wamekuwa wakweli na waaminifu,huwezi kumkuta DR.Shein kwenye dili ya vitambulisho vya TAIFA kama MEMBE,MASHA,LOWASSA n.k

au uzalendo na kufuata maadili ya kazi kwa MAREHEMU DR.OMAR ALI JUMA. ulinganishe na SUMAYE,LOWASSA,MRAMBA,YONA,MAGUFURI,MKAPA n.k

HAMAD RASHID HANA SPEA YAKE BUNGENI.
 
Kaka ndiyo tuseme Mengi ndiyo anaye sponsor Chadema? maana kwa mujibu wa RA yeye ni Nyangumi! kumbe heri nyangumi bora awe mchaga Khaa!
 


Zitto anataka kuvunga tu lakini ukweli ndio huu. Hata majibu yake yanaonyesha kama ameshikwa pabaya. Yaani anathubutu kukanusha kama Amani Kaboru hakuwa the man behind him katika kujikita kwenye siasa za CHADEMA.

Anakuja na hoja za ajabu eti alijiunga CHADEMA akiwa kidato cha tatu.... miaka 17. Mdogo wangu Zitto wake up. Mimi nakukubali sana kama mwana siasa. Lakini mwenendo wako wa siku za mwisho unaashiria the beginning of the end. Tena hasa pale ulipohitimisha kushawishi serikali kununua mitambo ya Dowans.

RA Hoye!
 
ninavofahamu mimi kwa historia iliyopo ukitoka Cuf kama umejilani mwenyewe.... kwa upande wa znz wananchi kule wana uhakika na baadhi ya watu wao ktk Cuf kwa upande wa znz
Ina maana CUF tu ndio inaweza kutetea maslahi ya ZNZ?
 


I agree with you totally! Wazanzibari meaning wote wa Pemba na Unguja tangu enzi ni watu waaminifu na waadilifu sana. Kama wapo ambao wamejiingiza kwenye masuala ya ulaghai na ufisadi watakuwa wanaiga kutoka Bara!

Hamad Rashid is a cool rational person, anaweza kuwa Rais mzuri na makini atakayeweza kuliokoa taifa hili kutokana na janga tulilonalo sasa hivi na kulirudishia Taifa heshima iliyokuwepo huko nyuma.
 

Hakuna sheria inayompa nafasi mtoto wa miaka 17 kuingia mkataba.uanachama wake ni batili.

hakuna anayeweza kupinga mchango wa Kaburu kwa Chadema,huyu ndiye aliyeipeleka Chadema Kigoma na kufanya watu wa familia moja kupigana kwa misingi ya CCM na Chadema labda mtu ambaye kaijua Chadema kupitia JF ndio anaweza kudanganywa.Alipokuwa Kaburu akihutubia mikutano ya Chadema na kampeni nzito,MBOWE alikuwa akishika mikoba ya Kaburu sembuse Zitto.
 

Vita yetu ni juu ya CUF kweli? hebu tumesahau kabisa adui yetu ni nani? kitendo cha kusema eti umefurahi ni unafiki na pia wewe ni mchekeshaji, sisemi vibaya ila dhamira inanisukuma kusema haya kuwa, vyama vya upinzani tunaitaji kusemea pamoja na si kubezana, tukisikia baya limekifika chama cha CUF tusikitike wote na wala si kuombeana mabaya.
 

Dah!! Kama ni kweli basi huyu ni miongoni mwa wanasiasa asiyependa ubunge!!! WAWI si Pemba? Kama ni Pemba sijui aamie chama gani atakachouzika kwavile jamaa hawachagui mtu bali Chama!!! Nazani anatakiwa kuzikumbuka KURA ZA MARUHANI kabla hajamua!!!
 
Dah!! Kama ni kweli basi huyu ni miongoni mwa wanasiasa asiyependa ubunge!!! WAWI si Pemba? Kama ni Pemba sijui aamie chama gani atakachouzika kwavile jamaa hawachagui mtu bali Chama!!! Nazani anatakiwa kuzikumbuka KURA ZA MARUHANI kabla hajamua!!!
HR hawezi kuhama CUF.
 


Umechemsha! walau ungeuliza basi alijiunga vp. Kwa ntaarifa Zitto kaingia Chadema katika umri huo (17) kupitia umoja wa vijana wa Chadema ambao sharti la kujiunga ni kijana mwenye umri wa miaka 12-17.

Rejea katika ya chadema sura ya tano 5.1.7


 
Last edited:
HR hawezi kuhama CUF.
Ah. Anahitaji kucheza karata zake hivi sasa. Na dume tayari analo mkononi-ile karata ya harufu ya K pia anayo. Sasa kama ataendelea kumsikiliza Maalim?
 
Mh hana lolote huyo anatikisa kiberiti,siku zote alikuwa wapi ,tutawaona na kuwasikia tena wakila matapishi yao,siasa ni mchezo wa kuigiza ndugu zanguni,wanasiasa hawaaminiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…