Hamas na Fatah wasaini mkataba wa kumaliza tofauti zao.Netanyahu amlaumu Mahmoud Abbas kwa hatua hiyo.

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Makubaliano yamefikiwa hii leo huko Beijing nchini China kati ya Hamas na chama cha Hamas ambacho kina mamlaka fulani huko ukingo wa magharibi.

Tangazo hili lilitolewa na waziri wa mambo ya nje wa China,ndugu Wang Yi ambapo upande wa Hamas uliwakilishwa na Mousa Abu Marzuk.Upande wa Fatah makubaliano hayo yalitiwa saini na waziri mkuu wa mamlaka hayo.

Makubaliano hayo ni pamoja na namna ya kulitawala eneo la Gaza siku ambapo itatangazwa vita vimesitishwa.
Baada ya kusikia tangazo hilo waziri mkuu wa Israel,Netanyahu ametoa lawama kwa kiongozi wa Palestina chini ya chama cha Fataha kwa kufikia makubaliano hayo na Hamas.

Hamas and Fatah sign agreement in Beijing ‘ending’ their division, China says

1721732576923.png
 
Waishukuru IDF japo kidgo basi maana bila kichapo Hamas - Fatah wangeendelea kutofautiana.

Hamas ndio bye bye tena mlipewa minofu mkatamani mifupa sasa hangaikeni nayo.
Wakipatana Hamas na Fatah na Israel nayo ndio kwisha kabisa.
Fatah ni uzembe wao tu lakini wana bunduki ndogo ndogo.Wakianza kuzitoa kuwapa Hamas hakuna setla atakayesogea kuchukua mashamba ya mezeituni ya wapalestina,
Na kama wamekubaliana kikamilifu basi anachofanya Hamas na Fatah hatolaumu wala kushika wapiganaji kuwatia ndani.
 
Hasa hasa ukishika wewe hizo bunduki, myahudi hatakanyaga Gaza, bila hivyo, hichi ni kichekesho kingine mkuu
 
Makubaliano yamefikiwa hii leo huko Beijing nchini China kati ya Hamas na chama cha Hamas ambacho kina mamlaka fulani huko ukingo wa magharibi.

Tangazo hili lilitolewa na waziri wa mambo ya nje wa China,ndugu Wang Yi ambapo upande wa Hamas uliwakilishwa na Mousa Abu Marzuk.Upande wa Fatah makubaliano hayo yalitiwa saini na waziri mkuu wa mamlaka hayo.

Makubaliano hayo ni pamoja na namna ya kulitawala eneo la Gaza siku ambapo itatangazwa vita vimesitishwa.
Baada ya kusikia tangazo hilo waziri mkuu wa Israel,Netanyahu ametoa lawama kwa kiongozi wa Palestina chini ya chama cha Fataha kwa kufikia makubaliano hayo na Hamas.

Hamas and Fatah sign agreement in Beijing ‘ending’ their division, China says

Hamas wameiponza gaza imeshaisha huko bora wawachie fatah watawale gaza
 
Wakipatana Hamas na Fatah na Israel nayo ndio kwisha kabisa.
Fatah ni uzembe wao tu lakini wana bunduki ndogo ndogo.Wakianza kuzitoa kuwapa Hamas hakuna setla atakayesogea kuchukua mashamba ya mezeituni ya wapalestina,
Na kama wamekubaliana kikamilifu basi anachofanya Hamas na Fatah hatolaumu wala kushika wapiganaji kuwatia ndani.
Fatah ni uzembe wao tu lakini wana bunduki ndogo ndogo 😱🙄:3Kool::ABDULpls::Concerned: astaghfirullah
 
Hakika mchina ni mtu mmoja smart sana.
Yani ndani ya muda mfupi ameweza kufanikisha jambo lililowashinda marekani na nchi nyingine za kiarabu kwa miongo kadhaa.
 
Mapatano ambayo yanaweza kuwasadia wapalestina ni mapatano ambayo yatahusisha arabs legue, kwa sababu hao ndio wanajua adha za wapalestina pia wanatambua kilichoko kwenye dini ya uislamu, uyahudi na ukristo kuliko China nchi ya mbali ambayo haiamini mambo ya dini ya uislamu, uyahudi na ukristo, huwezi kutenganisha migogoro ya middle East na dini hapo dini inahusika hasa uislamu, uyahudi na ukristo. Halafu China kuusuluhisha makundi mawili hasimu bila kuihusisha Israel bado ni Changamoto, maana yake anasuluhisha hamas na fatah ili watengeneze umoja wa kuishambulia Israel kwa pamoja. Je bila kumalizia tofauti zao na Israel Gaza itatawalika? China ilitakiwa ajikitee kutafuta amani na jinsi ya kumaliza vita kwa kuwashawishi hamas waachie mateka na Israel asitishe vita. Pia tukumbuke Israel imepoteza wanajeshi na raia kuliko mateka waliotekwa na Hamasi, Palestina imepoteza watu wengi , watu wamekufa wengi sana, na bado Israel ina wafungwa wa kivita wengi sana, hao wanaitwa ni wafungwa wa kivita lakini ni mateka wa kipalestina, kilichofanyika ni sawa na hamas wameteka 250 na kuua 1200, Israel amelipiza kwa kuteka 6000, kuua 40,000 na kuumiza 70,000, kuharibu Gaza kwa kiwango cha hali ya juu ambacho hakijawahi kutokea pale Gaza. Kwa calculation hizo wapalestina wamepata hasara kubwa sana.
 
Makubaliano yamefikiwa hii leo huko Beijing nchini China kati ya Hamas na chama cha Hamas ambacho kina mamlaka fulani huko ukingo wa magharibi.

Tangazo hili lilitolewa na waziri wa mambo ya nje wa China,ndugu Wang Yi ambapo upande wa Hamas uliwakilishwa na Mousa Abu Marzuk.Upande wa Fatah makubaliano hayo yalitiwa saini na waziri mkuu wa mamlaka hayo.

Makubaliano hayo ni pamoja na namna ya kulitawala eneo la Gaza siku ambapo itatangazwa vita vimesitishwa.
Baada ya kusikia tangazo hilo waziri mkuu wa Israel,Netanyahu ametoa lawama kwa kiongozi wa Palestina chini ya chama cha Fataha kwa kufikia makubaliano hayo na Hamas.

Hamas and Fatah sign agreement in Beijing ‘ending’ their division, China says

..."ametoa lawama"...! Katoa lawama zipi,kasemaje?
 
Huyo mchina kwanini asiwe msuluhishi kati ya urusi na ukraine
 
Waishukuru IDF japo kidgo basi maana bila kichapo Hamas - Fatah wangeendelea kutofautiana.

Hamas ndio bye bye tena mlipewa minofu mkatamani mifupa sasa hangaikeni nayo.
Haufaham kitu bwana mdogo. Haitawezekana kuanzisha/kulitangaza taifa la palestina kama Wapalestine wenyewe watakuwa na tofauti.

Hayo makubaliana yana maana kubwa sana kuna kitu hapo kinatengenezwa. Netanyau kaujua mchezo ndio maana anabweka
 
Israel imepoteza wanajeshi na raia kuliko mateka waliotekwa na Hamasi,
Ni ukweli ambao ni tamko la kushindwa kwa Israel katika vita.
Hilo halikuwa lengo lililotangazwa la vita vilipoanza.
 
Back
Top Bottom