Hamis Kiiza 'Diego' amwaga wino Simba!

Kuna mchezaji mmoja tu Yanga mwenye quality ya kuchezea Simba
Haruna Niyonzima
 
Nilikuwa namkubali sana huyo jamaa bas tu yanga tuliteleza tu
Mimi Nina makengeza (cross-eyed), na kwa hivyo ninawaona Kiiza wawili. Mmoja ni huyohuyo unayemwona wewe, kiungo mshambuliaji mwenye kasi anayemudu pia kucheza akiwa mshambuliaji wa kati, anayejua kufunga magoli na aliye mwiba kwa mabeki. Ni mshambuliaji anayefanya vyema zaidi kwenye mechi ngumu kama vile za watani wa jadi. Ni mshambuliaji ambaye kila kocha angependa kuwa naye, akiwamo kocha wa The Cranes.
lakini ninamwona Kiiza mwengine mtukutu kwa makocha, anayetaka achezeshwe bila ya kujali mipango ya mwalimu na kudhani ni dhambi yeye kutocheza dakika zote 90, hata asipohitaji kutumika kulingana na mfumo wa mwalimu au anayehitaji kuingia kama super-sub. Namwona Kiiza anayemhoji mwalimu kupitia vyombo vya habari kwa nini anawekwa ubao, Kiiza anayetolewa kumpisha mwenzake naye akafura kutorudi benchi na wachezaji wenzake, Kiiza ambaye (huenda kwa ila hizo) hakuwa chaguo la kwanza la Pluijm licha ya kupenda kwake washambuliaji wenye kasi. Kiiza ambaye hakuwa pia chaguo la Maximo (labda kwa tabia hizo na/au Ripoti ya Pluijm aliyemkabidhi Maximo). Kiiza ambaye licha ya kuachwa Yanga kwa mizengwe kama wengine wanavyoamini, akakaa mwaka mzima bila ya kupata timu. Kiiza ambaye (labda kwa huko kutokuwa na tiimu) hakuwa tena chaguo la kocha wa The Cranes.
Sasa sijui wenzangu mnamzungumzia Kiiza yupi!
 
Ni usajili mzuri. Ni mmaliziaji mzuri endapo atatengenezewa nafasi, sielewi kwa nini yanga walianza kumuweka benchi! Natumai atafanya mambo fresh!

Pale kati tulikua tunakosa mmaliziaji...Okwi alikua anatengeneza nafasi nyingi sana tatizo yule Danny alishindwa kuzitumia...Danny na Maguri ni wazito...

Kiiza ,Mgosi,ajib na Mavugo ni perfect choice
 
Pale kati tulikua tunakosa mmaliziaji...Okwi alikua anatengeneza nafasi nyingi sana tatizo yule Danny alishindwa kuzitumia...Danny na Maguri ni wazito...

Kiiza ,Mgosi,ajib na Mavugo ni perfect choice

hujamalizia na kaburu hans popo
 

Na mimi namwona Kiiza huyohuyo lkn nikiri wazi sikua nikifahamu kwa undani upande huu wa uliomalizia.
Lkn tukubali Kiiza ni mchezaji wa kiwango cha juu kwa soka la ukanda wetu na kwa kweli timu zetu huwa zinafanya makosa sana kuacha mbachao kwa msala upitao.

Yanga walifanya kosa kubwa kumwacha huyu na kumsajili Jaja na yule kiungo wa Kibrazil, lkn haliwezi kuonekana ni kosa kwa sababu Yanga ilikuwa na kikosi imara kilichofanya vzr na hakuna aliyejadili kwa kina kosa hili. Ni kama Simba na Tambwe, Simba hawataki kukubali kufanya kosa la karne!!!

Hizi timu tatizo zina wajuaji wengi na zinaendeshwa kwa bendera kufuata upepo, makocha nao wanakuja na malengo ya muda mfupi so wanawaza kama timu hizi hizi zinavyowaza.

Angalizo: Si kila mchezaji mzuri kutoka timu moja anaweza kufanya vizuri kwenye timu nyingine. Kiiza apewe muda na mpira hauchezwi kwa historia.
 
Kwani alipotoka hapo kwenye mafuriko alichezea timu gani_?
 
kiiza kwa mechi za mchangani anaziweza ila kwa za kimataifa haziwezi kwa iyo wazee wa mchangani anawafaa sana huyo
 
Nakubaliana mno na wewe. Ndio maana kwa misingi hiyohiyo ya hoja yako, ninapata mashaka na ufanisi wa siyo Kiiza tu, bali timu nzima ya Simba kwa msimu huu. Ni kubahatisha mno kukamilisha (au kukaribia kukamilisha) idadi ya wachezaji saba wa kigeni bila ya ushauri wa mwalimu. Mpira wa zama hizi unachezwa kwa mifumo. Wachezaji hutafutwa kwa mujibu wa mfumo ataoutumia kocha, sio kocha kutumia mfumo kwa wachezaji wa kutafutiwa. Tujaalie huyu wa Simba anatumia mfumo wa striker mmoja tu mbele, Simba itawafanya nini mastraika wataobaki nje kutoka jopo la akina Mavugo (iwapo atakuja kweli), Sserunkuma, Okwi, Diego? Na kwa bahati mbaya tuna kasumba kwamba mchezaji wa kulipwa kutoka nje hapaswi kuwa wa akiba, licha ya mifano hai ya akina Kaka wa Real, Czech wa Chelsea, n.k. Juu ya hao ongezea wazawa akina Ajib na Mgosi. Itakuwaje? Ndio hali hiyo hiyo iwapo atatumia mastraika wengi zaidi, akina Ndemla, Banda, Mkude (kama atabaki), Messi (kama atabaki) n.k. watafanya nini?Ndio maana sivutiwi na usajili wa Simba mwaka huu, na kwa hivyo bado siwapi nafasi kubwa ingawa hakuna taaluma ya kubashiri matokeo ya mpira. Naomba nieleweke, sina mana kwamba Simba hawajasajili wachezaji wazuri, la hasha. Nina maana kwamba kuna tofauti kubwa baina ya usajili mzuri na kundi la wachezaji wazuri. Kutengeneza upya timu inayotegemea wachezaji wengi wapya walio wa kigeni kwa kutumia kocha mpya aliye wa kigeni ambaye hakuhusika na usajili alioukuta ni kazi kubwa, inahitaji muda. Kwa hivyo wa kupewa muda sio Kiiza tu, bali mwalimu na timu nzima.
 


Naunga mkono hoja. Kwa mfano naona majukumu ya Mgosi na Kiiiza ni kama yale yale.

Kwa mtazamo wangu mm Simba hii iliyomaliza nafasi ya 3 msimu uliopita ilikuwa inahitaji wachezaji bora 3 kuifanya ipate mafanikio zaidi ya waliopata. Simba ilihitaji beki 1 wa kati aina ya Wawa wa Azam, ilihitaji striker wa kati bora na ambaye angeweza kutekeleza majukumu kama Sunzu wa enzi zake na kiungo mahiri wa aina na uzoefu wa Mwinyi Kazimoto.
Lkn pia Simba ilihitaji upana wa kikosi kwa maana ya kuwa na angalau wachezaji 18 wanaoweza kuwa kikosi cha kwanza na wanaoweza kuchukua nafasi ya walioko ktk kikosi cha kwanza wakati wowote wanaohitajika.

Tuliona Simba iliyopita ikisuasua pale ilipokosa baadhi ya wachezaji waandamizi hasa Okwi kwa hiyo tunaweza kuelewa ni kwa nini sasa hivi wamesajili aina ya wachezaji waliosajili nadhani ni kuwa na kikosi kipana kinachoweza kucheza msimu mzima bila ya kuwa na utegemezi uliopindukia kwa wachezaji wachache.

Kuhusu hoja ya mfumo, nadhani Simba hawana namna kwa sasa. Haya ni matokeo ya makosa au hali halisi ya kilichotokea huko nyuma.Kwa kitendo cha kuanza msimu bila kocha kila mara haya ndio matokeo yake, na kwa sasa hawawezi kuacha kusajili. Inabidi wasajili tu, kwa kuzingatia ushauri wa benchi la ufundi lililopita kama inavyodaiwa na kikubwa ni kutulia kuona timu inafanya nini. Na nataka kuamini watakuwa wamechagua kocha anaeendana na utamaduni wa Simba na kama sivyo basi itakuwa ni makosa mara mbili.
 
Mkuu Maftah hakufanya vizuri akiwa simba, nadhani simba ndo imempoteza maftah kwenye ulimwengu wa soka.
Mkuu Amir Maftah alicheza Simba kwa mafanikio na alikuwa akifanya vizuri sana, kama unakumbuka vizuri alimweka benchi Juma Jabu. Simba iliyoifunga Yanga goli tano Amir alikiwa beki tatu. Kilichomwondoa Simba sio kiwango bali ni kutoelewana na uongozi.
 
Kiiza ni winger? Sserunkuma alitokea ligi nyingine, alishindwa kubadilika kutokana na mazingira, kiiza ni tofauti, ila pia uwezekano wa kuwa flop upo!

Kiiza anacheza pembeni na kati....

Akiwa timu ya taifa ya vijana alikuwa anachezeshwa kati...

Kwenye ngazi ya vilabu ikiwemo enzi zake Yanga amekuwa akichezeshwa pembeni...

Binafsi bado naamini Sserunkuma ni mchezaji mzuri kuliko Kiiza...

Hadi leo sijajua kwa nini alishindwa kucheza uzuri hapo Simba...
 

nakubaliana nawe kwamba Simba hawakuwa na namna kwa sasa ila kusajili kwa kubahatisha. Lakini hilo haliwavui lawama ya ukosefu wa umakini. Kuna wakati walikuwa na namna ya kuepukana na hali hiyo. Hawakupaswa kwa tofauti ndogo tu ya fedha kukosana na kocha aliyekwishawaonesha uwezo na aliyekwishakubalika kwa wachezaji/wanachama/wapenzi. Kwa maoni yangu, fedha inayotumika kwa 'kurundika' wachezaji kadhaa wanaofanana uwezo na majukumu (mf. Mgosi na Kiiza kama ulivyosema) au hata kuajiri kocha mahsusi wa viungo ambaye kwa timu inayoshiriki ligi ya nyumbani pekee angeweza kuajiriwa kwa vipindi vifupivifupi tu, zingetosha kuziba nakisi ya alichohitaji kocha Kopunovic. Huku Visiwani tunasema usiwache kunasua (aliyekwishanasa) kwa kutega. Ndicho walichofanya Simba. Walipaswa kubwia kiburi chao kwa kumridhia Mserbia yule, kuliko kuanza na kocha asiye na uzoefu wa kuwa kocha mkuu na ambaye wasifu wake unaonesha kuwa anahama timu mbili ndani ya msimu mmoja. Labda kama wamevutiwa na kasi hiyo inayofanana na yao katika kubadili makocha. Maana Waswahili husema 'hogo halihogoki ila kwa hogo jenziwe', na kwamba 'pwagu (jizi la kupindukia) hupata pwaguzi (jizi lililopindukia zaidi) nalo likapwaguliwa.'
 
Naomba kuweka kumbukumbu sahihi.. "fundi" hamis kiiza a.k.a diego si kapi, maana aliondolewa na maximo, ili jaja aweze pata nafasi.

Ombi lako la kuweka kumbukumbu sawa limekataliwa kwani na wewe umekosea pia.

Jaja alisajiliwa mwanzo wa msimu wa ligi kuu uliopita chini ya coach Maximo. Mchezaji aliyempisha Jaja anaitwa Emmanuel OKWI aliyejipeleka Simba baada ya Yanga kunuia kumuacha kwenye mataa dakika za lala salama za usajili. Kiiza aliendelea kuwepo Yanga hadi muda ulioamuliwa ulipowadia.

Kiiza aliachwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili akimpisha Kpah Sherman chini ya Coach Pluijm.

Mkuu sembo mbona siku hizi unakoseakosea sana, vipi, kukosa ubingwa, umakamu bingwa na kujikita mchangani kumekuchanganya hadi leo?
 
Last edited by a moderator:
Kweli dunian tumekuja kuishi hatujaja kufanana kimaisha.yanga tunasajili ngoma,simba wanamsajili kiiza!kweli nafasi ya tatu ni ya kwenu simba kwa usajili huu.
 
Hiyo siyo tetesi bali ni kweli Hamis Kiiza kasajiri Simba SC jioni hii.My take:Hakuna mchezaji aliye wahi kutoka Yanga kwenda Simba akapaform vzr.Unawakumbuka hawa?LUNYAMILA,MMACHINGA,MATHIAS MULUMBA,MAFTA JNR N.K.Jee Kiiza atabadirisha upepo?

Acha historia za kipuuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…