Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Hamis Lisu, mmoja wa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Ikungi, mkoani Singida, ameamua kutogombea ubunge wa jimbo la Singida Magharibi.
Uamuzi huo umetokana na kile alichosema kuwa mbunge wa sasa, Elibariki Kingu, ametekeleza vyema wajibu wake kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo hilo.
“Nashukuru mbunge kwa kuniita hapa, lakini nilivyoona vumbi lilivyotimka, nikajiuliza nina ubavu kweli? Ubavu wa kupambana na huyu bwana (Kingu) ninao kweli?” alisema Lisu. Aliongeza kuwa aliomba wale waliokuwa wanamshawishi achukue fomu washindwe na walegee.
Pia soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Lisu pia alionyesha kutokubali kuwania, akijua kuwa siasa ipo katika damu yake, lakini alisisitiza kuwa amefanya uamuzi wa busara kutokana na mambo makubwa yaliyofanywa na viongozi wa CCM pamoja na upendo wao kwa wananchi.