Hamis Mwinjuma (Mb), ameshiriki zoezi la ugawaji wa medali kwa timu zilizofanya vizuri kwenye finali za mashindano ya Kimataifa ya shule za Sekondari

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (Mb), ameshiriki zoezi la ugawaji wa medali kwa timu zilizofanya vizuri kwenye finali za mashindano ya Kimataifa ya shule za Sekondari Barabi Afrika yaliyofanyika Durban nchini Afrika Kusini ambapo Tanzania iliwakilishwa na timu ya wasichana ya Fountain Gate Dodoma High School waliotwaa ubingwa wa mashindano hayo kwa upande wa wasichana.

Zoezi la ugawaji wa Medali hizo liliongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe, Mawaziri wa Michezo kutoka nchi washiriki wa mashindano hayo pamoja na marais wa mashirikisho ya mpira Afrika ambapo Tanzania ikiwakilishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma (Mb) na Rais wa TFF, Wallace Karia.View attachment 2581439View attachment 2581440View attachment 2581442View attachment 2581443View attachment 2581441View attachment 2581444
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…