Hamisa Mabetto akiri kuwa anapenda wanaume matajiri

Hamisa Mabetto akiri kuwa anapenda wanaume matajiri

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Hamisa Mobetto kila mara amekuwa akizungumziwa mno na kudaiwa kuwa mwanamke aliye na tabia chafu ya kulala na kuzaa na wanaume matajiri.

Kulingana na mwanamitindo huyo raia wa Tanzania, halalamiki kwa sababu malezi ya watoto wake ni bora na baba zao wana mkwanja wa kutosha.


Kupitia ujumbe mpana wa Instagram ambo TUKO.co.ke ilitupia jicho Jumapili, Septemba 2, mama huyo wa watoto wawili alisema kuwa, baba za watoto wake wana jukumu na watafanya kila wanaloweza kuhakikisha anaishi maisha anayotaka.

"Nilimpata mwanangu wa kwanza miaka kadhaa iliyopita na nashukuru katika uhusiano wangu nilipendwa na kushughulikiwa. Hata baada ya kumzaa mtoto wangu wa pili, nilishughulikiwa inavyofaa na ninapenda kuwashukuru baba za watoto wangu," alisema.

Zari Hassan, kila mara amekuwa akimponza mno mwanamitindo hiyo kwa kuwa na tabia ya kujihusisha katika mapenzi na matajiri na kuwatumia watoto wake kama kitegauchumi.

Licha ya vijembe vya Zari, Hamisa kila mara ameshikilia yeye ni mfanyabiashara ambaye haitaji mwanamume kumtunza.

Lakini sasa amekiri mwenyewe kwa kwenda kinyume na kauli yake ya awali dhidi ya vijembe vya Zari.

Kuna kipindi Mobetto alimburuta Diamond Platnumz ambaye ni mzazi mwezie kortinikwa sababu ya malezi ya mtoto wao.

Katika ujumbe wake, mwanamitindo huyo pia aliwaomba msamaha maadui zake na kusema hana muda tena wa kupapurana nao mtandaoni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nlitaka kuuliza ni nani huyo... Nmesoma kumbe ni mwanamke. NYIE WANAWAKE HAMPENDANI KABISA. sasa unakuja kutushirikisha na sisi wanaume watu hata hatuwafahm.sis majiran au mashoga zako tutawafahamia wapi mama?
 
Back
Top Bottom