Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Microsoft wameachia feature mpya kwa watumiaji wa windows 10 na windows 11 kuweza kuhamisha files lolote toka kwenye simu kwenda kwenye kompyuta bila waya, Unatumia mfumo wa wireless tu kuweza kuhamisha vitu.
Feature hii inaitwa show mobile device in files Explorer inakupa uwezo wa kuona file zako zilizopo kwenye simu na kuonekana kwenye kompyuta kupitia files Explorer na kukupa uwezo wa kuhamisha chochote utafikiri Unatumia USB kumbe ni wireless.
🧿KWENYE SIMU
🛡️ Pakua app ya link to windows app toka play store
🛡️ Ifungue kisha sign na akaunti yako ya Microsoft ambayo Unatumia kwenye kompyuta
🛡️ allow permission zote watakazo kuomba kisha malizia setup.
🧿 KWENYE KOMPYUTA
🛡️ Ingia setting kwenye kompyuta yako
🛡️ Tafuta sehemu ilipoandikwa Bluetooth & device
🛡️ Kisha ingia sehemu ya Mobile Device malizia kwa kubonyeza sehemu ya Manage device utagusa sehemu ya ku sign In.
🛡️ Chagua akaunti yako ya Microsoft ambayo ume signed kwenye simu ukimaliza sasa utaona neno "Show mobile device in files Explorer"
Utaweza kuweka On baada setup kuwa completed fungua sasa File explorer kwenye kompyuta yako chini ya This PC utaiona simu yako utaweza kuhamisha chochote unachotaka.
KUMBUKA
Mfumo huu unaanzia kwa watumiaji wa simu za android version 10 na kuendelea🙃.