Hamjambo kweli?

KEFODAW

Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
34
Reaction score
2
Enyi wapenda amani wenzangu, poleni sana kwa majukumu mengi ya kila siku. Tafadhali hebu fanya kila liwezekanalo kila mmoja kwa nafasi yako ilimradi kauli hizi za kibabe kati yetu na jirani zetu Rwanda zisituingize kwenye hali tuliyoiona wakati wa vita kati yetu na Uganda mwaka 1978. Kauli aliyoitoa kiongozi wetu kuwa ...tutamshughulikia kama tulivyomshughulikia nduli Idd Amin, si njema na wala hazina maana kuwa sisi watanzania katika ile vita tulibakia salama tu wala hatukudhurika. Mimi naamini kwamba kuwa kimya na makini kuna manufaa makubwa kuliko kutamba kuwa tutampiga kama tulivyofanya kwa Idd Amin enzi hizo. Nayasema haya kwa kuwa nataka wasioelewa hili waelewe kwamba vita kati yetu na Rwanda haitakuwa vita ya nchi hizo mbili tu. ni wazi kuwa tutajikuta tunapigana na nchi nyinginezo ambazo nitazitaja kesho.
 
Karibu sana JF....
Kesho si ndio leo...zitaje basi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…