Hammer Q Aibuka na 'Kazi na Dawa'

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
MSANII mahiri wa muziki wa taarabu nchini, Hussein Mohamed 'Hammer Q', ameanza rasmi kazi ndani ya kundi la Five Star kwa kuibuka na wimbo wake mpya uitwao 'Kazi na Dawa'.
Hammer Q ambaye alianza kutamba kwenye taarabu akiwa na kundi la Dar Morden Taarab kutokana na nyimbo zake za Gharika la Moyo na Siri ya Penzi, alijiunga na Five Star katikati ya mwaka huu, lakini alikaa kimya bila ya kutoa wimbo.

Msanii huyo ambaye alipanda chati na kuwa miongoni mwa waimbaji taarabu wa kiume wanaopendwa zaidi akiwa Dar Morden, alisema'Kazi na Dawa' utamrudisha kwenye chati ya juu pindi utakapoanza kupigwa kwenye redio na televisheni.

"Huu ndio ukweli wenyewe. Mimi ndiyo muimbaji hivyo najua uzito wa nyimbo hizi tatu. Ubora wa Kazi na Dawa ni tofauti na ule wa 'Kitu Mapenzi' na Gharika la Moyo, huu uko juu zaidi," alisema Hammer Q.

Msanii huyo alisema kuwa uwezo mkubwa aliouonyesha katika wimbo huo unatokana na hasira aliyonayo kwa viongozi wa Dar Morden wanaotangaza kuwa yeye (Hammer Q) si mchapakazi.

"Walikuwa wanasema mimi si mfanyakazi, sasa wimbo wangu wa kazi na dawa utawanyamazisha midomo yao. Nataka kuwaonesha kuwa mimi ni msanii wa ukweli" alisema Hammer Q.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…