Hamna mkoa nimewahi kwama kwenye utafutaji kama Singida

Hamna mkoa nimewahi kwama kwenye utafutaji kama Singida

The Eric

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
6,446
Reaction score
10,976
Daaah walio toboa kwenye huo mkoa hongereni. Daah mikoa mingine utasema upo KENYA siyo Tanzania.

Licha ya ugumu wa pesa hali ya hewa pia haikunifurahisha upepo mkali, maji chumvi daah, jua kali sana, viwanja vyao vipo na mawe, chakula cha shida pale, wamezoea ugali na mboga za mlenda. Wadada wao sasa hata kupika hawajui, wazuri ila hawana matunzo kabisa yaani afu washamba.

Wanyaturu na wanyiramba samahanini🙌🙌🙌 Sijui wachagga wanapataje pesa pale maana asimili 85% ya wafanyabiashara wa ule mkoa wakubwa ni wachagga tena wa kibosho wengi. Wazawa wengi wako kwenye alizeti na vitunguu.

Naamini ipo mikoa mingine kama Singida walio ambulia zero pia. Serikali iangalie namna Singida nao wapate wamezungukwa na mikoa yenye tija wao wapo kati wanafyta mikia.

Wewe umewahi ishi wapi pakakuchosha, yaani hukupata chochote.
 
Kuna mikoa migumu sana kiutafutaji hususani ile ambayo imekaliwa na wazawa kwa wingi mfano Lindi Singida nk ogopa unaenda mkoa unakuta wazawa wanajadili huyu atakuwa ni kabila fulani mikoa ya kiutafutaji inajulikana mkuu Dar, Mwanza, Mbeya ila Arusha sio sana.
 
Kuna mikoa migumu sana kiutafutaji hususani ile ambayo imekaliwa na wazawa kwa wingi mfano Lindi Singida nk ogopa unaenda mkoa unakuta wazawa wanajadili huyu atakuwa ni kabila fulani mikoa ya kiutafutaji inajulikana mkuu Dar, Mwanza, Mbeya ila Arusha sio sana.
Acha tu mkuu yaani wanyaturu wanakoroga kikwao kama wapo kwenye maalizeti, utasikia wacha worewa mnyampaa. Upo town kati kama kijijini.
 
Lima Alizeti Ama Uza Mawe
Utaazia wapi mtaji huna ndiyo umefika mjini unazamia tu. Saa hizo Unaranda kama chinga. Alizeti siyo mchezo usubiri ikue wewe upo shambani, utakula nini?

Kitu kina washinda watu kilimo ni kusubiri huku muda wako uko shambani. Swali huo muda utakuwa unapata wapi fedha za kujikimu, ndiyo maana unaona vijana wanakuwa machinga kwa mitaji midogo waliyo nayo kama ni elfu 20 au 50 twende kazi. Shida ni mzunguko amna unaanza kula mtaji na faida ya siku za nyuma.

Kitaa banaa nimeranda.
 
Acha tu mkuu yaani wanyaturu wanakoroga kikwao kama wapo kwenye maalizeti, utasikia wacha worewa mnyampaa.
Upo town kati kama kijijini.
Unaenda mko unafungua biashara yako lakini unashangaa mbona wateja sipati!!? Kumbe watu wameshaambiza huyu mwenye duka sio mwenzetu,, kinachofuata ni kifunga biashara huku ukiwa na hasara kibao.
 
unaenda mko unafungua biashara yako lakini unashangaa mbona wateja sipati!!?
kumbe watu wameshaambiza huyu mwenye duka sio mwenzetu,,
kinachofuata ni kifunga biashara huku ukiwa na hasara kibao
Eeeh ipo hivyo mkuu kuna baadhi ya mikoa ipo hivyo mfano singida wanyiramba wana hako katabia....

Tena ufungue biashara ya mgahawa utakimbia, labda uuze bidhaa ambazo hazina ubaguzi.
 
Habari yako mkuu.. pole kwa hayo, wewe ulikuwa unajishugulisha na biashara gani apa singida kwetu
Niliuza nguo wakati huo za mtumba zikagoma, nikarudi kwenye matunda napo holaa!!!!! viatu navyo nikauza holaa!!!! Nikaambiwa viatu subiri Sikukuu ya Idd au wakivuna vitunguu daaah nikaona nitakuwa nakula nini....

Serikali haijapeleka hata vyuo vya kueleweka pale mkuu yaani ni uhasibu tu tena tawi la TIA ndiyo lipo pale. Labda kuna VETA tu pale.
 
Eeeh ipo hivyo mkuu kuna baadhi ya mikoa ipo hivyo mfano singida wanyiramba wana hako katabia....

Tena ufungue biashara ya mgahawa utakimbia, labda uuze bidhaa ambazo hazina ubaguzi.
Hili nalikataa tena wewe umeenda miaka hii singida kuna lami kila kona. Nilianza kazi wilaya ya Iramba awamu ya kwanza ya JK kuko choka mbaya hakufai kuishi mtu na asilimia kubwa ya watu wenye hela na miradi mikubwa ni Wachaga wangewakataa wasingekuwa wengi vile
 
Back
Top Bottom