Hamna mwanaume mzuri kama mimi!

huyo ana matatizo kama sio walakini aliöna wapi mwanaume rijali akijisifu kwa uzuri
 
<br />
<br />
Bujibuji hapa umenifanya nivunjike mbavu.
 
Mwanaume anayekuwa na simu ya Blackberry na wale wanaovaa suti na tai huku wameshika magazeti huwa sitaki hata kukutana nao.

Ha ha ha ha sasa huyu ana Blackberry nne??????????? Halafu mzuri mbona vichekesho duniani humu
 
Igwe mbona umeshangaa. Hao ndio wanaume wanajiita wazuri sasa sijui na wanawake watasemaje

hili ni jipya kidogo mkuu,....kumbe wale masharobaro wanaoigiza wanamaanisha,......mmmmmmmh
 
Mwanaume anayekuwa na simu ya Blackberry na wale wanaovaa suti na tai huku wameshika magazeti huwa sitaki hata kukutana nao.

Ha ha ha ha sasa huyu ana Blackberry nne??????????? Halafu mzuri mbona vichekesho duniani humu

Mimi nina N8,navaa suti bila tai na huwa sishiki magazeti kamwe, sura yangu ni ya kokoto.....je!...ntapata nafasi
 
Huyo katoka mombasa. Alipoona kule kasifiwa kuwa mzuri kajua na huku atasifiwa na kubabaikiwa.
 

Mpe hongera zake
 
Niko full Booked

sawa sawa_nilifikiri haujabahatika kukutana na wenye sura ya kokoto_ambao ndio chaguo lako anyway,......mwambie rafiki yako kama vp,napatikana mkoa mpya wa katavi
 

wanaume wa siku hizi...
- wanapaka poda
- wanapaka lip gloss
-wanapenda kulelewa na mijimama
kubwa kuliko wanajisifia kuwa wao ni
wazuri...tena wazuri kuliko wanaume wote

huko tuendako mmmmmmh... kazi ipo
 

wanaume wa siku hizi...
- wanapaka poda
- wanapaka lip gloss
-wanapenda kulelewa na mijimama
kubwa kuliko wanajisifia kuwa wao ni
wazuri...tena wazuri kuliko wanaume wotehuko tuendako mmmmmmh... Kazi ipo

waambie wabadili tabia
 
mh!!! huyu vip uzuri wa mwanaume uko kenye mshiko bwana,huyu ana biashara zake zingine.
 

Anaweza kuwa yuko sahihi. Ungemwuliza anaposema mzuri ana maana gani. Inawezekana ni mzuri kwa mujibu wa vigezo anavyotumia yeye kijipima.
 
jamani kichaa kina viwango hivyo msishangae sana, huo ni mwezi mchanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…