Hamna namna mbadala ya kuomba ajira Seriaklini bila kupitia ajira portal?

Hamna namna mbadala ya kuomba ajira Seriaklini bila kupitia ajira portal?

Frank Hood

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2021
Posts
597
Reaction score
1,374
Naomba nijue, naona siku hizi ukitaka kuomba kazi za Serikali unapitia ajira portal(www.ajiraportal.gov.tz).
Sasa swali langu inakuwaje kwa wale ambao wako uko vijijini au hawana access ya internet wanafanya vipi kupata hzo ajira? Maana hawatoi alternative way ya kutuma maombi zaidi ya kupitia ajira portal.

Kama kuna alternative tufahamishane

Na hii ajiraportal ukisahau password na kuomba link ya kufanya password reset haikuletei hiyo link kwa hiyo ni kama inakuwa imekula kwako vile coz hutoweza kujisajili tena kwa mara ya pili ina maana hutoweza kuomba tena ajira za Serikali na institution zake, utapiga simu na kuomba msaada kupitia namba zilizowekwa lakin simu hazitopokelewa na zikipokelewa utazungushwa hadi utachoka.

Sasa ni nini lengo la hii ajira portal kama chngamoto zake hazifanyiwi kazi?maana ukiacha nilizozitaja ila bado ina changamoto nyingi sana kitu kwakweli kinachokera
 
Back
Top Bottom