Hamna pesa rahisi online, jua hilo

Hamna pesa rahisi online, jua hilo

Kaunara

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
249
Reaction score
452
Vijana hata watu wazima wengi bado wanaimini kuna kazi au pesa rahisi unaweza pata kupitia simu yako au kuwa online.

Chini ya hili jua hamna pesa rahisi. Pesa halali ni ile ya kuitolea jasho. Kama kuna mtu Tanzania hii analea familia yake na anasomesha watoto wake na online money aje aseme hapa.

Watanzania hamna mtu analea familia kwa betting, au casino games mwanzo mwisho. Watu wanakuwa na source nyingine ya income ndo anacheza hivi vitu bila pressure. Kwaiyo hata akikosa bado anakipato chake. Hii dhana vijana wanashinda kwenye hii michezo asubuhi hadi jioni na amini tutapata vichaa wengi sana huko badae.

Hamna online platform yeyote ile itakupa hela zaidi we ndo utawapelekea hela. Kuna biashara nyingi sana za kufanya na kuna kazi nyingi sana halali za kufanya. Shida ipo watu kuchagua kazi.

Kama umesoma tuliza akili angalia wapi unaweza toboa. Watu wanakimbilia mimi sina mtaji mimi sina mtaji. Ila ukweli ni kwamba wewe mwenyewe ni mtaji tayari.

Matajiri wengi wameanza na kuthubutu. Angalia Diamond, azam na wengine wengi wamehangaika sana. Kutukanwa mbele za watu kuaibishwa kuonekana hawana akili wanapoanza ila leo hii ni watu wa heshima.

Sasa wewe jifungie na simu yako chumbani ukisema unatafuta hela. Au shinda kwenye macasino ukisema kuna hela utapata siku moja. Kweli utapata hatukatai ila sio kila siku. Fungua hata banda la chipsi tu kama unaamini kwenye mambo ya online hij inamaana hata ukikosa huko una mahali unaweza pia ishi.
 
Jaribu kubadilisha mtazamo , pesa hupatikana kwa kutumia akili na ubunifu kwa dunia ya sasa.Wewe bado upo katika dunia iliyopita ya kutumia nguvu na kuajiriwa! Unahisi kutoka jasho ndiyo kupata hela au kuendelea kuwa mtumwa??
Ndo huko kutolea jasho.
 
Kuna waliobahatika hizo pesa za online wanapata na wanaendesha maisha yao na wanatajirika kuanzia hao content creators n.k
Hata biashara kuna ambao wanafilisika na kuna wanaofanikiwa..
Hatukatai ila ni wangapi kwa mwaka wanakuwa matajiri? Weka hapa.
 
Vijana hata watu wazima wengi bado wanaimini kuna kazi au pesa rahisi unaweza pata kupitia simu yako au kuwa online.

Chini ya hili jua hamna pesa rahisi. Pesa halali ni ile ya kuitolea jasho. Kama kuna mtu Tanzania hii analea familia yake na anasomesha watoto wake na online money aje aseme hapa.

Watanzania hamna mtu analea familia kwa betting, au casino games mwanzo mwisho. Watu wanakuwa na source nyingine ya income ndo anacheza hivi vitu bila pressure. Kwaiyo hata akikosa bado anakipato chake. Hii dhana vijana wanashinda kwenye hii michezo asubuhi hadi jioni na amini tutapata vichaa wengi sana huko badae.

Hamna online platform yeyote ile itakupa hela zaidi we ndo utawapelekea hela. Kuna biashara nyingi sana za kufanya na kuna kazi nyingi sana halali za kufanya. Shida ipo watu kuchagua kazi.

Kama umesoma tuliza akili angalia wapi unaweza toboa. Watu wanakimbilia mimi sina mtaji mimi sina mtaji. Ila ukweli ni kwamba wewe mwenyewe ni mtaji tayari.

Matajiri wengi wameanza na kuthubutu. Angalia Diamond, azam na wengine wengi wamehangaika sana. Kutukanwa mbele za watu kuaibishwa kuonekana hawana akili wanapoanza ila leo hii ni watu wa heshima.

Sasa wewe jifungie na simu yako chumbani ukisema unatafuta hela. Au shinda kwenye macasino ukisema kuna hela utapata siku moja. Kweli utapata hatukatai ila sio kila siku. Fungua hata banda la chipsi tu kama unaamini kwenye mambo ya online hij inamaana hata ukikosa huko una mahali unaweza pia ishi.

“Hakuna pesa rahisi popote”
 
Ndo huko kutolea jasho.
Amini amini nakwambieni hakuna pesa rahisi online lakini kuna pesa za kufanyia kazi online.
Shida inakuja pale mtu anapoamini kwamba kuna pesa ya kudownload.
Kuna really work zinafanyika remotely online na watu wana earn more than mshahara wa watu wengi hapa tz.
Kuwa tajiri unaweza usiwe tajiri kaa sababu utajiri ni mind set, je unachokipata una kiinvest? Maana bila hivyo unaweza ubaki ulivyo. Kuna watu wamewahi kuwa wabunge lakini wakafulia kabsa baada ya ubunge.
Japokuwa you have to work hard, pia work smart na uwe tayari kujifunza mambo mapya. Dunia ya sasa iko kasi na mabadiliko ni kila siku.
Online pesa ipo na mimi ni shuhuda wa hilo. Lakini si ya kudownload kama watu wanavyosema.
 
Hii kitu inalipa ni namna ya kuiotea tu nimethibitisha hilo, usishangae jamaa yako anakamilisha pagala lake akaezeka bati na kupiga vioo aluminium finishing ya nguvu ukahisi amechukua mkopo bank, ni risk ila inalipa ukiiotea
 
Mimi BINAFSI na bet ila aisee naliwa Zaid kuliko kula so nikamua tu niwe mfugaji once nikila hata laki nakimbilia kununua vikuku VINGI Yani naitakatisha ile hela..kitu ambacho sifanyi ni eti kuuza kuku ili nifanye deposit betpawa Yani bora hela nyingine kbs ndo niifanyie huo utumbo kamari
 
Kama waliwa zaidi kuliko unavyokula hata ukinunua kuku ni bado hasara.
 
Hii kitu inalipa ni namna ya kuiotea tu nimethibitisha hilo, usishangae jamaa yako anakamilisha pagala lake akaezeka bati na kupiga vioo aluminium finishing ya nguvu ukahisi amechukua mkopo bank, ni risk ila inalipa ukiiotea
Hamna kitu hapo
 
Kama waliwa zaidi kuliko unavyokula hata ukinunua kuku ni bado hasara.
Ni kweli ndo maana mkuu nachofanya kwa mfano nimepata laki tano posho kazini..natenga laki moja nanunua kuku laki mbili nampa wife kwa ajili ya home laki moja nalipa madeni halafu laki moja ndo naifanyia utumbo naweka betpawa so hapo najaribu bahati ila mara nyingi najikuta imeliwa ..so nikiona nimeishiwa natulia kimya najifanya kamari ni haramu mpk nipate hela nyingine kbs ya kazi ..ila siwezi kuthubutu eti nipate hamu ya kuweka match za UEFA na Sina hela nikakamate kuku niuze hiyo never
 
Hapo bora hujawa na addiction iliyopitiliza
 
Nadhani bado hujajua Google inalipa watu kiasi gani kwa mwezi, ni millions of $$
 
Ni suala la muda tu kila mtu ataanza kuongea mwenyewe
 
Back
Top Bottom