Hamna watu wanaotapelika kirahisi kama waumini wa dini hii

Hamna watu wanaotapelika kirahisi kama waumini wa dini hii

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001

Sijajua ni kwa nini baadhi ya Wakristo wamekuwa wakisadikishwa na kuaminishwa na wao haraka haraka huamini na mwishowa siku hujikuta wakiwa mateka wa kifikra.

Visa vingi sana tumeviona na tumevishuhudia vya watu kuuziwa kijifuko cha chumvi tu hii ya dukani kwa shilingi laki moja huku wakisadikishwa kuwa inaleta utajiri na kumfukuzia mbali pepo mchafu alitaye ufukara.

Tumeona watu wakisadikishwa kuwa ukipada mbegu utavuna lolote ulitakalo, mathalani, unataka kuwa Mkurugenzi wa Bandari, au unataka kuwa daktari mkuu na wewe elimu yako ulikomea darasa la nne A, basi panda mbegu, inenee na wewe utavuna jambo ulitakalo.

Wakristo wameaminishwa kuwa kina St. John, St. Peters, St. Richard na wazungu wengine waliokufa zamani ndio wanaweza kutuombea.

Mizimu ya kizungu, wala haikujui je inawezaje kukuombea? Mizimu ambayo haina hata uhusiano na wewe?

Omba kupitia mizimu ya kwenu, achana na hao wahuni wa kimagharibi, wanachotaka kutoka kwako ni sadaka tu.

Wanahubiri upendo na hawana upendo, hata marehemu Benjamin Williams Mkapa alichana na upadre baada ya kuona huko kwenye mission kumejaa gjiriba, chuki , ubaguzi na upendo haukuwepo.

Mapadre wazungu walikuwa wakiwanyanyapaa na kuwaona mapadre weusi kama takataka halafu wakipanda madhanahuni wanajidai wanahubiri upendo.

Hizi dini zichunguzeni kwa kina, kisha zirekebiswe huenda zikawa bora kidogo
 
Inalingana tu na kupewa BIKRA 72 peponi na mito ya pombe za kila aina unajichotea tu.
Bongo utakuta mtu anaitwa Mohammed Juma Abdullah anakwambia hana jina la ukoo lenye asili ya kwao, lakini huko Afrika Magharibi waislam wana majina asili kabisa kama NGOLO KANYE, SADIO MANE etc, Bongo tunaona utamadani wa watu ndio ujanja
 
Inalingana tu na kupewa BIKRA 72 peponi na mito ya pombe za kila aina unajichotea tu.
Eti ungali hai unakatazwa usitumie pombe na usiwe mzinzi, lakini cha ajabu ukishakata umeme unaruhusiwa kutumia vyote, inabidi uzimie uzinduke kama mara trilioni hivi ndipo utaweza kuelewa huo mstari [emoji1787]
 
Inalingana tu na kupewa BIKRA 72 peponi na mito ya pombe za kila aina unajichotea tu.
Hivyo bikra 72 umetoa kifungu gani? Kuhusu pombe hata biblia imezungumzia siku ya mwisho kutagongwa vyombo


Mathayo 26:29 BHN​

Nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”

Hapa mada kwa nini mnatapeliwa kirahisi? Usihamishe mada
 
Back
Top Bottom