Hamonize: Wewe ni kioo cha jamii, jiheshimu acha mdomo mchafu

Mabel

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2010
Posts
1,276
Reaction score
684
Bila kuwachosha, moja kwa moja kwenye maada.

Jana nimekutana na Hamonize kwenye ndege toka Nairobi kuja Dar (KQ486), kwa maongezi yao na aliokuwa nao inaonekana alitokea SA.

Kilichonikera toka kwa huyu bwana ni mdomo mchafu, anatoa maneno machafu bila kujali kwenye ndege ile kuna watu wazima wenye busara zao. Alikuwa na dada mmoja akafikia hatua ya kumwambie aache kutukana.

Wasanii nyie ni kioo cha jamii, siyo sawa kuwa na tabia za kihuni bila kujali mazingira na watu mlionao kwa wakati huo.

Mwisho, nendeni shule itawasaidia katika mziki wenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…