Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HAMU MPYA YA KUMFAHAMU ABDUL SYKES NA HISTORIA YA TANU
Kumekuwa na mwamko mpya wa kushangaza kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Juma lililopita tukielekea Nyerere Day nimekuwa nikihojiwa na televisheni takriban kila baada ya siku na wakati mwingine siku zikifukuzana mfululizo.
Ajabu ya Rahman hawa vijana wameshikwa sana na historia ya mchango wa Abdul Sykes katika kuasisi chama cha TANU.
Nimewauliza kama hawachoki kuwaonyesha watazamaji wao historia hii kwani kila ajae kwangu hatakosa maswali kuhusu Abdul Sykes na TANU.
''Mzee Mohamed sisi tunasikiliza hotuba za Baba wa Taifa kila siku usiku sasa miongo miwili baada ya kufa kwake na Mwalimu Nyerere anahutubia taifa na hatujachoka kumsikiliza.
Historia ya Abdul Sykes hatukupata kusomeshwa hata vyuoni sasa tuna kiu nayo.
Kwani wewe unaona tabu kuihadithia?''