Wana jamii wenzangu naombeni mnijuze, mwenzenu nimekuwa na hamu ya kula udongo mara kwa mara. Mimi nina chofahamu ni kuwa hamu ya kula udongo inatokana na mtu kuwa mjamzito lakini mimi si mjamzito ila natamani kula udongo na nimekuwa naula sana kuanzia mwezi uliopita. Nifanyeje niache kula udongo na je una madhara gani katika mwili wa binadamu?