mtanzania asiye jielewa
Senior Member
- Nov 13, 2016
- 179
- 98
Ndugu zangu nilikuwa nasumbuliwa na tatizo la mkojo kutoka kidogo kidogo yaani kila nikienda chooni mkojo hauishi. Nikaenda hospitali ya rufaa nikapimwa wakanikuta nina UTI sugu, nikaandikiwa sindano saba lakini tatizo halijaaisha kila dakika ni kwenda chooni mkojo unatoka kidogo unakata mpaka imefikia hatua nimekata tamaa.
Sasa leo nikiwa nimechoka huku maumivu yakizidi pale unapoanzia uume ikabidi nijishike kwa kupangandamiza ndipo nilisikia kitu kimenikata kwa ndani nikashtuka sana hapo hapo mkojo ukanibana nikakimbia kwenda chooni sijui kipi kimenituma nikojoe nje ya sink la chooni. Wakati mkojo unatoka kwa kasi na mimi nikijikamua NILISIKIA KITU KIMETOKA KWENYE UUME WANGU ndipo nikainama nikalisafisha na kuliokota kuangalia kwa makini ni mawe kama matatu yameeungana ndipo nikalipeleka hospitalini (maabara) mtu wa maabara alishangaa sana akaenda kuliangalia aliporudi aliniiuliza je hukutoka damu? Nikamjibu hapana wakaniomba nipeleke mkojo.
Kwa hiyo kesho ndo nitaenda kuchukua mjibu kamili.
Swali langu kwenu wataalamu, ni kwanini hali hii imenipata?
NAOMBENI MAJIBU NDUGU ZANGU