Hamza Aziz na karabai za misikiti ya Kariakoo 1940s

Mpaka sasa waongo wanaoshikilia rekodi hap JF ni wewe na Yeriko
kidudu vibaya hivyo, mzee na kaka yetu mo'hd anajitahidi kutujuza mambo ya dar miaka ile bila gharama yoyote ww unamkejeri,Mungu hachelewi kuwaadhibu wenye dhihaka kama ww,tubu tafadhari.
 
Nnangale,
Sijui huyu ndugu yetu ni kipi kimemghadhibisha katika yale niliyoandika kiasi cha kunifedhehesha.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwa na nyumba Mtaa wa Mbaruku jirani na nyumba ya Aziz Ali baba yake Hamza Aziz.

Baba yangu akifahamiana na wote katika familia yao na ndiyo sababu ya ukaribu huu wangu na Hamza Aziz.
 
Ok ndio mwenye mtaa pale kwa azizi ali mtongani
 
Kusali,kuswali amua moja acha unafiki
 
kidudu vibaya hivyo, mzee na kaka yetu mo'hd anajitahidi kutujuza mambo ya dar miaka ile bia gharama yoyote ww unamkejeri,Mungu hachelewi kuwaadhibu wenye dhihaka kama ww,tubu tafadhari.
Hata mimi nampenda Mzee Mohamed kwa historia zake za jiji la Dar Es Salaam lakini tatizo lake kubwa ni udini,historia zake zinakuwa za kuwaenzi watu ambao ni wa dini ya Kiislam na huu ni ubaguzi ambao hata katika maandishi ya vitabu vitukufu yanapinga,sisi sote ni waja wa mwenyezi Mungu,hakuna aliyezaliwa Muislamu au Mkristo,hizi dini tunarithi tu kutoka kwa wazazi kwa hiyo sio dhambi kuwa mkiristo au mwislamu au usie na dini.Tunataka huyu mzee aongelee maisha na historia ya Dar Es Salaam bila kuegamia upande mmoja,najua atasingizia kuwa ah wakazi wengi wa Dar Es Salaan na mikoa ya pwani toka enzi hizo wengi wamekuwa Waislamu,swali je unapoongelea mambo ya maisha ya jiji la Dar Es Salaam lazima uislamu uingizwe ?ni sawa na kusema basi tunapoongelea kwa mfano London au Washington lazima tuingize ukristo au makanisa badala ya kuzungumzia kwa mfano reli za chini zilivyojengwa au watu walivyokuwa wanateseka.Mzee Mohamed kweli ni nguli wa historia na simulizi na hata uandishi wake ni wa kutukuka unaposema unapata raha lakini angekuwa kama marehemu Shaabani Robert.
 
mfianchi uandishi wako ni wa hekima sana,anachojaribu kufanya bw mkubwa Mo'hd ni kuandika upande ambao haukuandikwa vya kutosha,nabado kwenye simulizi zake kawataja akina John Rupia (lupilya)akina Nyerere,Dr kyaruzi,Makalanga na wengine ingawa kusudi lake mara zote ni kuonyesha juhudi za waislamu kupambania uhuru wa nchi yetu hiyo inatokana na historia anavyo ijua yeye na anavyoona waislamu hawapewi uzito wanaostahili.kimsingi kaka Mo'hd anaungana na mzee seleman Takadiri kimuono.
 
kaka taa ya kandili ya nini msikitini wakati msikiti unapangaboi?
 
sasa unalalamika lalamika umeme unakatika,kwani mnashindwa kununua jenereta?
 
Msome vzuri Mzee Mohamed Said amekuwa akiandika khs historia ya Tanzania kiujumla lazima tukubariane wapingania uhuru wa nchi hii wengi wao walikuwa waislam ss uwezi kuandika bila kuwapa sifa zao khs upande wa pili wapo pia moja moja km mzee wetu John Rupia Max mbwana chief maliale nk...
 
Historia nzuri... Umenifanya nifahamu wanini mtaa wa kwa Azizi Alli.... Je waweza fahamu huyu mzee wakidigo alifika Dsm mwaka gani? Na elimu yake ya engineer wa majengo alisomea wapi?
 
Quigley,
Aziz Ali
ni baba yake Dossa Aziz na Hamza Aziz.

Hapo kwa Aziz Ali ndipo akiishi baba yao na wana hodhi kubwa sana
na ndipo yalipo makaburi yao.
Kama bado wanahodhi sehemu kubwa bado,ikawaje Dossa akiishi kifukara Mlandizi?
 
Mkuu Mohamed Said inabidi usichoke kutufundisha historia ya nchi yetu,kuna vijana wamezoea uongo hao ukisema ukweli watauita uongo.Ni bahati nzuri kwamba tunawajua nao wanajua kwamba wanajulikana.Ukweli husimama wenyewe ña Wala hauhitaji bunduki ,mabomu na lift.Waliozoea kukaririshwa historia za kutengeneza ili kulinda matumbo yao usiwajali sana.
 
kaka taa ya kandili ya nini msikitini wakati msikiti unapangaboi?
Nnangale,
Taa ya kandili kwa ajili ya kuangaza umeme unapokatika.

Pangaboi kwa ajili ya kupepea sijafamu vipi umehusisha vitu hivi viwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…