Hamza Kassongo on Sunday: Mazungumzo na Mohamed Said

Hamza Kassongo on Sunday: Mazungumzo na Mohamed Said

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HAMZA KASSONGO ON SUNDAY ETV "MCHAKATO WA UHURU" SAA TATU USIKU 27 DECEMBER 2020

Dudu...
Nashukuru sana kwa kutazama vipindi nilivyohojiwa.

Kuna kipindi kingine nimefanya, "Hamza Kassongo on Sunday," ETV kitarushwa In Shaa Allah Jumapili ijayo saa tatu usiku, "Mchakato wa Uhuru."

Kipindi cha saa nzima tunazungumza historia ya kujikomboa kuanzia African Association 1929 hadi kuundwa kwa TANU 1954.

Utapata fursa ya kusikia historia ya wazalendo ambao hawafahamiki sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika kama Hamza Kibwana Mwapachu, Rashid Ali Meli, Ali Mwinyi Tambwe, Iddi Faiz Mafungo, Robert Makange na Rashid Kheri Baghdelleh, Chief David Kidaha Makwaia, Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Hawa bint Maftah, Earle Seaton, Schneider Plantan na wengine wengi.

20201222_164225.jpg
 
Mzee Muhamed.Kitakuwepo you tube?Ningependa nisikie nondo zako.Nafikiri ni wakati sasa wa kuanza kuichukulia historia yetu kwa uzito wake hasa kwa kuzingatia kwamba tunaishi katika zama ambazo mwenye taarifa sahihi ndo mwenye mali.
 
Mzee Mo said

Nashauri hayo mazungumzo yawe online YouTube Ile nasisi tusio angalia television tuwezi kufuatilia kwa umakini zaidi.
 
Mzee Mo said

Nashauri hayo mazungumzo yawe online YouTube Ile nasisi tusio angalia television tuwezi kufuatilia kwa umakini zaidi.
Rhz...
Wenye mamlaka hayo ni ETV.
Hii station kwangu ni mpya sijui mipango yao.
 
Back
Top Bottom