kuna mambo kadhaa hapa kaka ambayo yanakupelekea kuwa hivo ulivo:-
1. inawezekana kabisa kuwa nyumbani mna ugomvi ambao ni wa mda mrefu na hamjaupatia suluhisho na hivo kitu fulani kimekukaa moyoni na ndo mana unaona hakuridhishi japo anafanya kile anachotakiwa kufanya lakini wewe huoni.
2. inawezekana umepata mwanamke wa nje, tatizo la binadamu wakipata watu kama hawa, (awe mwanamke au mwanamme), huwa kuna kuwa na ile kasumba ya kipya kinyemi...wengi sana huwa tunafanya makosa tukiwa na watu kama hawa kwa kujaribu kulinganisha utendaji wao hawa watu na wake zetu wa nyumbani, lakini sio sawa na sio sahihi kulinganisha, kwa vyovyote tu mara nyingi utaona kipya kizuri zaidi.... kwani shati jipya na lile la zamani lipi linakuvutia zaidi kaka?. Hii sababu ya pili mimi ndo naipa nguvu sana.. na kama ndio acha huyo anayetaka kukuharibia nyuma maana ukimchukua na baadae ukapata kifaa kipya kingine mambo yatakuwa ni yale yale.
3. inawezekana wewe bwana ni chovya chonya, unapenda kuonja kila mwanamke na hivyo ukakutana na tofauti baina yao...binadamu hawafanani kaka na ndivyo ilivyo, na kwa kuwa mkeo unae kila dakika mnatazamana kila leo, mnananihiuuu kila siku unaona umeshamchoka..kwani umemzoea, jua kuwa tatizo la kuchokana katika ndoa sio kwako wengi linawasumbua na tu kwa sababu hawajajifunza kuwa kwenye ndoa kuna uwezekano wa kuchokana hivyo kutafuta njia mbadala ya kukabili hali hiyo inapotokea na kuifanyia kazi...
Ninachoweza kukuambia kaka, ufanyayo ni ya muda mchache na usidhani kwa kumuacha mkeo itakuwa suluhisho...kama unadhani ni suluhisho jaribu utakuja kutupa ushuhuda hapahapa jf baada ya miaka kadhaa, kama unazo..achana na nyumba ndogo zitakuharibia mengi tu, mrudie mungu wako, kaa na mkeo umwambie haya unayotuambia kwa hekima na mtafute wapi mmeteleza mrekebishe..
vitabu vya mungu vinasema, "Mwanamke Mpumbavu huaribu nyumba yake kwa mikono yake" mimi naongeza "hata mwanaume mpumbavu " vivo hivyo", hope utazingatia haya